Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua meneo yaliyoathika kwa mafuriko katika kijiji cha Gendabi wilayani Hanang, Disemba 4, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Muonekano wa mai wa Kateshi ambao baadhi ya mitra imejaa tope. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alitemblea eneohilo Disemba 4, 2023
Muonekano wa mai wa Kateshi ambao baadhi ya mitra imejaa tope. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alitemblea eneohilo Disemba 4, 2023
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua meneo yaliyoathika kwa mafuriko katika kijiji cha Gendabi wilayani Hanang, Disemba 4, 2023.
***********
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasili wilaya ya Hanang mkoani Manyara na kukutana viongozi wa mkoa huo na wa Serikali na kupokea taarifa ya hali halisi ya tukio la maafa lililotokea jana na kusababisha vifo na majeruhi.Waziri Mkuu alitoa pole kwa viongozi na wananchi wa Hanang kwenye kikao kilichofanyika leo (Jumatatu, Desemba 4, 2023) kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, vyombo vua ulinzi na usalama na Watendaji wa taasisi za Serikali.
Waziri Mkuu amesema tukio la jana linafanana na tukio jingine lililowahi kutokea mwaka 1990 katika eneo la Ndanda ambako mlima uliporomoka na kusomba nyumba na barabara, hali ambayo ilisababisha vifo na majeruhi.
Amezishukuru Kamati za Maafa za Wilaya na Mkoa ambazo zilianza kuchukua hatua za uokoaji tangu jana, lakini pia mawaziri na watendaji wao ambao walikuja kutoa msaada kwa kuungana na viongozi wa mkoa wa Manyara.
Amesema matibabu yanaendelea kutolewa kwa majeruhi ambapo timu ya madaktari bingwa kutoka Dodoma, Singida na Arusha imeungana na kuanza kutoa huduma za upasuaji kwa wagonjwa watatu waliovunjika mifupa.
Amesema majeneza yameagizwa kutoka Babati na Singida ili ndugu waliotambuliwa waweze kuhifadhiwa kwenye nyumba zao za milele.
Hivi sasa, Waziri Mkuu na baadhi ya mawaziri wamekwenda kukagua eneo la Mlima Hanang kwa kutumia helikopta. Eneo hilo ndiko maporomoko ya udongo yalianzia. Baadaye atashiriki kuaga miili ya marehemu na ndipo taarifa rasmi itatolewa.
0 comments:
Post a Comment