Jeshi la Polisi mkoa wa Songwe linawatafuta watuhumiwa wa kosa la kuharibu mali katika kijiji cha Halungu-Mbozi.
Ni kwamba Disemba 18, 2013 huko kata ya Halungu wilaya ya Mbozi mkoani Songwe shamba la mahindi lenye ukubwa wa heka 11 lililolimwa na watu 04 walilokodi kwa Edina Mgala, shamba hilo alilikodisha kwa kuligawa kwa watu hao ambao ni Mailo Msangawale (35) alikodishiwa heka 07, Emi Magwaza (48) alikodishiwa heka 1.5,
Salome Nkota (50) alikodishiwa heka 1.5, na Jeremia Ngoya (42) alikodishiwa heka 1 wote ni wakulima na ni wakazi wa Halungu.
Heka hizo zimeharibiwa baada ya kupuliziwa dawa ya kuulia magugu aina ya Rounup na mtu/watu wasiofahamika.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa ardhi unaohusisha familia mbili kati ya watoto wa mke mkubwa na mke mdogo wa marehemu Focus Makonongo.
Jeshi la Polisi mkoa wa Songwe kwakushirikiana na maafisa kilimo wilaya ya Mbozi linafanya tathimini ili kuweza kujua dhamani halisi ya mali iliyoalibiwa pamoja na kemikali iliyotumika kufanya uharibifu huo.
Jeshi la Polisi mkoa wa Songwe linatoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za mtu au watu ambao wamehusika katika tukio hilo ili waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Aidha Jeshi la Polisi mkoa wa Songwe linatoa rai kwa wananchi kutokujichulia sheria mkononi badala yake kutatua migogoro kwa kukaa vikao na kusuluhisha kwa amani.
Imetolewa na
THEOPISTA MALLYA- ACP
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Songwe.
0 comments:
Post a Comment