Nafasi Ya Matangazo

November 24, 2023

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo  mkoani Iringa ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi ya kuzungumza na  kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi hao.
Mtumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa, Felister Mnyawami akizungumza mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati alipotoa nafasi ya watumishi hao kuzungumza changamoto zao zinazowakabili ili aweze kuzitafutia ufumbuzi.
Sehemu ya watumishi wa Halmashuri ya wilaya ya Kilolo wakimsikiliza  Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete alipokuwa akizungumza nao ambapo ameahidi kushirikiana nao katika kutatu changamoto mbalimbali zinazowakabili
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo  mkoani Iringa ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi ya kuzungumza na  kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi hao.

Na Lusungu Helela- Kilolo
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete amesikitishwa na wimbi kubwa la wafanyakazi hususan walimu  wanaotuma maombi ya kutaka kuhama katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, Mkoani Iringa.


Mhe.Kikwete ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Watumishi wa Halmashuuri ya Kilolo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya  kikazi Mkoani humo ya  kuzungumza na kusikiliza kero za  watumishi na kuzitafutia ufumbuzi.

Amesema Watumishi walio wengi wanaotaka kuhama wamekuwa wakitaja sababu zinazofanana jambo ambalo lina walakini huku akisema kuna matatizo ya kiuongozi katika Halmashauri hiyo .

Ametaja moja ya sababu zinazopelekea  Watumishi hao kutaka kuhama ni pamoja na kupuuzwa na  kutokusikilizwa pindi watumshi hao  wanapokuwa na changamoto.

'" Kuna watumishi hapa hawajapandishwa vyeo kwa muda miaka tisa na wengine hapa licha ya kujiendeleza kielimu mishahara yao haijabadilika lakini ninyi Maafisa Utumishi wenye jukumu la kufuatilia UTUMISHI  na kuwapa majibu mpo tu, hili sio sawa hata kidogo" amesisitiza Mhe.Kikwete.

Amefafanua kuwa katika Halmashauri hiyo Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala wamekuwa miungu watu  badala ya kuwa suluhisho la matatizo yanayowakabili watimishi wanaowasimamia.

Amesema licha ya watumishi wengi wanaotaka kuhama kutaja sababu inayofanana,  kuwa ni uwepo wa baridi kali na hivyo kusumbuliwa na "athma" jambo ambalo si kweli, ukweli ni kwamba hakuna mahusiano mazuri kati ya Watumishi na Uongozi wa Halmashauri hiyo.

Kufuatia hatua hiyo Mhe.Kikwete amemtaka  Mkurugenzi kufanyia kazi changamoto zinazowakabili watumishi hao ikiwemo kufanya vikao vya mara kwa mara na watumishi  kwa ajili ya kuwasikiliza pamoja na kuzingatia stahili zao ikiwepo posho za likizo.

Katika hatua nyingine Mhe.Kikwete amewatak Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala kuwa kimbilio la watumishi badala ya kuwa vikwazo katika kufanyia kazi changamoto za watumishi.

" Kazi yenu Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala ni kusikiliza, kupendekeza watumishi wenu katika kupandishwa vyeo lakini mlio wengi mmekuwa ni watu wenye roho mbaya na mnaopenda kuwakomoa wenzenu, acheni hizo " amesisitiza Mhe.Kikwete

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo, Estomin Kyando ametumia nafasi hiyo kumshukuru Naibu Waziri Kikwete kwa kufika kwa ajili ya kuzungumza na watumishi anawaongoza huku  akiahidi kufanyia kazi maelekezo yote aliyoyatoa ili watumishi waweze kufurahi kufanya kazi katika Halmashauri hiyo.
Posted by MROKI On Friday, November 24, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo