Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu akizungumza na wawakilishi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO's) yanayojihusisha na masuala ya Mazingira ambapo aliwataja kukutana na kufanya tathmini ya namna Utunzaji Mazingira unavyotekelezwa Jijini Dodoma kwa kila robo ya Mwaka wa Fedha.
Mwenyekiti wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Bi. Mwantumu Mahiza amewasisitiza viongozi wa taasisi hizo kuzigeuza taka kuwa malighafi kwa kutumia Teknolojia tofauti tofauti zilizopo ndani ya nchi.
************
Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu ameyataka Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO's) yanayojihusisha na masuala ya Mazingira kukutana na kufanya tathmini ya namna Utunzaji Mazingira unavyotekelezwa Jijini Dodoma kwa kila robo ya Mwaka wa Fedha.
Bw. Gugu amesema hayo leo Oktoba 23, 2023 katika kikao kazi cha Utunzaji wa Mazingira kwa mashirika hayo yaliyopo Mkoani Dodoma kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Jengo la Mkapa.
"Sisi viongozi wa Dodoma hatutofautiani na ninyi ndio maana tunapongeza juhudi za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali yake kwakuwa karibu sana na Taasisi ambazo ziko nje ya Serikali kwasababu mnao mchango mkubwa katika kuyalinda Mazingira yetu.
Mkutano huu ni fursa ya kutambuana na kujua shughuli zinazofanywa na kila mmoja wetu. Tutakuwa tukikutana kila robo ya Mwaka wa Fedha ili kuweza kujadiliana na kufanya tathmini ya kazi zinazofanyika kwenye Mkoa"
Aidha Bw. Gugu amewaasa wadau mbalimbali wa Mazingira Mkoani humo kushirikiana kwa kuwa dhamira ya taasisi hizo ni kuhakikisha Mazingira yanatunzwa na kuhifadhiwa vizuri.
Naye Mwenyekiti wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Bi. Mwantumu Mahiza amewasisitiza viongozi wa taasisi hizo kuzigeuza taka kuwa malighafi kwa kutumia Teknolojia tofauti tofauti zilizopo ndani ya nchi.
Kikao kazi hicho kimezihusisha mashirika hayo yasiyo ya kiserikali yanayojihusisha na Utunzaji na Usafi wa mazingira kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma huku lengo kuu likiwa ni kujadili na kuweka mikakati inayohusiana na Mazingira hususani katika Makao makuu ya nchi.
0 comments:
Post a Comment