Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), CPA Hosea
Kashimba, (katikati), akimuhudumia mwanachama wa Mfuko huo, Bi. Happiness
Kusaga, wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja kwenye makao makuu ya
PSSSF, jijini Dodoma Oktoba 3, 2023. Wengine pichani kutoka kushoto ni
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bw. Paul Kijazi, na Mkurugenzi wa
Uendeshaji Bw. Mbaruku Magawa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), CPA Hosea Kashimba amezindua maadhimisho ya PSSSF ya wiki ya Kimataifa ya Huduma kwa Wateja Oktoba 3, 2023, Jijini Dodoma.
Akizindua maadhimisho hayo kwa upande wa PSSSF, CPA Hosea Kashimba ameungana na watumihi wa Mfuko huo kutoa huduma kwa wateja (wanachama) waliofika kwenye ofisi za PSSSF na kisha kuwapatia zawadi za kumbukumbu ikiwemo miche ya matunda.
Mmoja wa wanachama aliowahudumia na kisha kumkabidhi mche wa mti ni Bi. Hapiness Kusaga.
Kampeni hiyo iliyozinduliwa hivi karibuni na PSSSF ina lengo la kuunga mkono juhudi za serikali za kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya tabianchi.
Wakati wa uzinduzi huo, CPA Kashimba amewashukuru watumishi wa PSSSF kwa kufanya kazi kwa bidii, kuimarisha ushirkiano baina yao ambao umechochea kutoa huduma bora; na ubunifu wao uliosaidia mabadiliko makubwa kwenye huduma.
CPA Kashimba ametoa hamasa kwa watumishi kuendelea kujituma na ameahidi kutoa motisha kwa watumishi watakaojiongeza na kutoa ushirikiano mzuri. Maadhimisho ya Kimataifa mwaka huu yana kaulimbiu isemayo "Team Service"; inayohimiza ushirikiano wa watendaji wote kwenye utoaji wa huduma maridhawa.
Maadhimisho hayo yameshuhudiwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji Mbaruku Magawa, Meneja wa Huduma Laila Maghimbi na watumishi wa Idara ya Huduma kwa Wateja iliyoko Makao Makuu.
Maadhimisho ya Wiki ya Kimataifa ya Huduma kwa Wateja yanaadhimishwa duniani kote kila wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba kuunga mkono juhudi za watoa huduma katika kutoa huduma na suluhisho la huduma.



.jpg)
.jpg)













0 comments:
Post a Comment