Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya akikagua moja ya gari linalotengenezwa katika Karakana ya Wakala wa Ufundi na umeme (TEMESA) Tabora.
Muonekano wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Vijijini linalojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), katika kijiji cha Mwambaha
Kaimu Meneja wa TANROADS mkoa wa Tabora Eng. Christerphola Nichombe akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya alipokagua barabara ya Tabora- Mambali –Bukene-Itobo inayojengwa kwa kiwango cha lami. **************
Na Lucas Raphael,Tabora
Mameneja wa Wakala wa Barabara
nchini (TANROADS), Wametawakiwa kuhakikisha
barabara kuu na za mikoa nchini kote hasa sehemu za korofi, mitaro na
madaraja yanasafishwa na kuimarishwa ili kukabiliana changamoto zinazoweza
kusababishwa na mvua za vuli zinazotarajiwa kuanza kunyesha msimu huu wa
masika.
Raia hiyo ilitolewa jana na
Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey
Kasekenya alipokuwa akikangua maendeleo
ya ujenzi wa Barabara ya Tabora-Mambali-Bukene ambayo ujenzi wake kwa kiwango
cha lami unaendelea katika maeneo korofi kabla ya mvua kuanza kunyesha .
Alisema kwamba kipindi cha
masikia barabara nyingi zimekuwa zinakata wamawsiliaono na zingine kuharibika
kutoakana na kutochukua taadhari na kuziona mvua ni kidogo .
Naibu Waziri Mhandisi
Kasekenya alisema upo umuhimu wa wajenzi
na wasimamizi wa barabara kufuatilia na kufanyia kazi taarifa za utabiri wa
hali ya hewa zinazotolewa na mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA).
“Habari zinasema mvua za vuli
zinatarajiwa kunyesha katika kiwango cha juu ya wastani hivyo ili kuepuka
mafuriko, kukatika kwa barabara na madaraja ni vema kila meneja katika mkoa
wake akajipanga mapema kukabiliana na changamoto zitakazojitokeza ili
kutoathiri huduma za usafiri na uchukuzi”, alisema Mhandisi
Kasekenya.
Kwa mujibu wa TMA kati ya
mwezi Oktoba hadi Disemba maeneo mengi ya mikoa ya Kagera, Geita,Mwanza,
Shinyanga, Simiyu,Kigoma, Dar es salaam, Pwani, Morogoro na Tanga yanatarajiwa
kupata mvua za juu ya wastani na wastani.
“Mikoa ya Arusha, Manyara na
Kilimanjaro inatarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani hivyo
umakini na utayari wa kukabiliana na mvua hizo pale zitakapoleta madhara kwenye
miundombinu unahitajika ili kuondoa usumbufu kwa wasafiri”, alisisitiza naibu waziri
huyo wa ujenzi.
Katika hatua nyingine Naibu
Waziri Kasekenya ametoa siku 14 kwa Mtendaji mkuu wa TEMESA kufuatilia
ukarabati wa karakana ya TEMESA mkoani Tabora ili kujiridhisha kama unakwenda
sambamba na malengo ya Serikali ya kuboresha karakana hizo nchini.
“Tunataka karakana za TEMESA
ziwe za kisasa kimuonekano na kwa huduma zinazotolewa ili kuendana na kasi ya
serikali ya awamu ya sita” alisema Mhandisi
Kasekenya.
Posted by MROKI
On Wednesday, September 27, 2023
No comments
0 comments:
Post a Comment