Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameteuliwa rasmi kuwa Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Kituo cha Dunia
cha Uhimilivu wa Mabadiliko ya Tabianchi (Advisory Board of the Global Centre
on Adaptation - GCA).
Taarifa ya uteuzi huo
iliwasilishwa na Mhe. Ban Ki-moon, Mwenyekiti wa Bodi ya GCA na Katibu Mkuu
Mstaafu wa Umoja wa Mataifa alipokutana na Mhe. Rais pembezoni mwa Mkutano wa
Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika Nairobi, Kenya.
Heshima hii ni utambuzi wa uongozi mahiri wa Rais Samia katika jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya
tabianchi Afrika na duniani kote ambapo Tanzania ni kinara kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali barani Afrika.
Wajumbe wengine wa Bodi hiyo ni Rais wa Jamhuri ya Senegal Mhe. Macky Sall, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa
Afrika Mhe. Moussa Faki
Mahamat, Rais wa
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Mhe.
Akinumwi Adesina na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) Mhe. Kristalina Georgieva.
GCA ni taasisi kubwa duniani inayosimamia masuala ya uhimilivu wa
mabadiliko ya tabianchi, ambapo hadi sasa imeweza kufanikisha upatikanaji zaidi
ya Dola za Marekani bilioni 50. Tanzania ni miongoni mwa nchi za kwanza
zitakazonufaika na fedha hizo katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment