Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt.Doto Biteko akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Ihako wilayani Bukombe Mkoa wa Geita mara baada ya kuwasha umeme katika Kijiji hicho tarehe 26 Septemba, 2023.

Moja ya nyumba iliyounganishwa na umeme katika Kijiji cha Ihako wilayani Bukombe mkoani Geita.
Teresia Mhagama na Godfrey
Lulinga
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko ameanza kazi ya kuwasha umeme vijijini ambapo leo amewasha umeme katika Kijiji cha Ihako, wilayani Bukombe mkoani Geita na hivyo kuwezesha wananchi katika kijiji hicho kuanza kutumia rasmi nishati hiyo.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji hicho, Dkt.
Biteko amepongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kazi nzuri ya kupeleka umeme vijijini ikiwemo kijiji cha Ihako na kuelekeza kuwa,
sasa mwendo ni wa mchakamchaka kupeleka umeme kwa wananchi wote waliopo
vijijini.
"REA nendeni vijijini, muda wa kufanya
vikao kwenye maukumbi makubwa au makao makuu ya miji hatutaki, tunataka tuwaone
mnaenda vijijini kupeleka umeme, nyie ni Wakala wa Nishati Vijijini siyo Wakala
wa umeme mijini , vikao vyenu viwe na wananchi na magari yenu yapite humo wanamopita
wananchi wenye maisha ya kawaida kabisa, " amesisitiza Dkt. Biteko
Ameongeza kuwa, Serikali inataka kuona shuguli
za kupeleka na kuwasha umeme vijijini zinatokea, na kwamba umeme huo uingie
kwenye nyumba zote bila kubagua kwani kila mwananchi anahitaji umeme.
Aidha ameelekeza kuwa, mahali penye changamoto
za umeme zitatuliwe kwa haraka na si kumsubiri, Rais, Dkt. Samia Suluhu
Hassan kutatua changamoto wakati wa
ziara zake wakati wasaidizi wake wapo.
Amesema kuwa fedha za kupeleka umeme vijijini
zipo ambazo zimechangiwa na wananchi, Serikali na wadau wa maendeleo hivyo
hakuna sababu ya kukwamisha miradi ya umeme nchini.
Kuhusu nishati safi ya kupikia, amesema
kuwa, Serikali inataka ione wananchi
wanatumia nishati hiyo na kwamba REA
waweke mpango ili mitungi ya gesi iwafikie
wananchi wa kawaida nchini na hivyo kuwaondolea matumizi ya nishati ambayo si
salama.
Vilevile amesema kuwa,
Serikali inafanya jitihada mbalimbali ili kupata umeme wa kutosha kutoka vyanzo
vya umeme ikiwemo Mradi wa Julius Nyerere ( MW 2115) ambao utaongeza kiasi
kikubwa cha umeme
kwenye gridi ya Taifa na hivyo wadau wa umeme watapata umeme wa kutosha ikiwemo viwanda, wachimbaji wadogo na wenye shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi
Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy, amesema kuwa, Mkoa wa Geita una jumla ya
Vijiji 461 ambapo vijiji 399 sawa na asilimia 86.6 vimepata huduma ya umeme
kupitia miradi ya REA Awamu ya Tatu mzunguko kwanza, REA Awamu ya Pili na REA
Awamu ya Kwanza.
Amesema kuwa, REA inaendelea
kutekeleza miradi mbalimbali mkoani Geita ambapo wakandarasi wapo maeneo ya
miradi wanaendelea na kazi na kuitaja miradi inayoendelea kuwa ni REA Awamu ya
Tatu Mzunguko wa Pili, mradi wa kupeleka umeme pembezoni mwa miji Awamu ya Tatu
, mradi wa kupeleka umeme kwenye migodi midogo na maeneo ya kilimo pamoja na mradi
wa kupeleka umeme kwenye vituo vya afya na pampu za maji.
Captions
Moja na Mbili
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt.Doto Biteko akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Ihako wilayani Bukombe Mkoa wa Geita mara baada ya kuwasha umeme katika Kijiji hicho tarehe 26 Septemba, 2023.
Moja ya nyumba iliyounganishwa na umeme katika Kijiji cha Ihako wilayani Bukombe mkoani Geita.
***************
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko ameanza kazi ya kuwasha umeme vijijini ambapo leo amewasha umeme katika Kijiji cha Ihako, wilayani Bukombe mkoani Geita na hivyo kuwezesha wananchi katika kijiji hicho kuanza kutumia rasmi nishati hiyo.
kwenye gridi ya Taifa na hivyo wadau wa umeme watapata umeme wa kutosha ikiwemo viwanda, wachimbaji wadogo na wenye shughuli mbalimbali za kiuchumi.

0 comments:
Post a Comment