Nafasi Ya Matangazo

August 04, 2023

Muonekano wa Jengo la Makazi la Kibiashara la Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), lenye sakafu 11 na uwezo wa kuhudumia kaya 22, lililopo katika makutano ya barabara  ya Kinana na Afrika Mashariki eneo la Sekei, jijini Arusha
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akipata maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Daud Kondoro wakati wa hafla ya ufunguzi wa jengo la makazi la kibiashara lililopo katika makutano ya barabara  ya Kinana na Afrika Mashariki eneo la Sekei jijini Arusha. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa jengo la makazi la kibiashara lililopo katika makutano ya barabara  ya Kinana na Afrika Mashariki eneo la Sekei, jijini Arusha. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikata utepe kuashiria Ufunguzi wa Jengo la Makazi la Kibiashara la Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) lililopo katika eneo la Sekei Jijini Arusha leo tarehe 04 Agosti 2023. Wengine katika picha ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof Makame Mbarawa, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula, Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela, Mtendaji Mkuu wa TBA Arch. Daud Kondoro pamoja na wawakilishi wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango pamoja na viongozi wengine wa Serikali wakifungua pazia kuashiria ufunguzi wa jengo la makazi la kibiashara lililopo katika makutano ya barabara  ya Kinana na Afrika Mashariki eneo la Sekei, jijini Arusha. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akipokea tuzo ya heshima kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Daud Kondoro wakati wa hafla ya ufunguzi wa jengo la makazi la kibiashara lililopo katika makutano ya barabara  ya Kinana na Afrika Mashariki eneo la Sekei, jijini Arusha.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Majengo (TBA), Arch. Dkt. Ombeni Swai, katika hafla ya ufunguzi wa jengo la makazi la kibiashara lililopo katika makutano ya barabara  ya Kinana na Afrika Mashariki eneo la Sekei, jijini Arusha. 
Sehemu ya viongozi mbalimbali wa taasisi na mashirika waliohudhuria hafla hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof Makame Mbarawa pamoja Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula katika sebule ya moja ya nyumba iliopo katika Jengo la Makazi la Kibiashara la Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) lililopo katika eneo la Sekei Jijini Arusha mara baada ya kufungua jengo hilo leo tarehe 04 Agosti 2023.

***********
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amefungua jengo la makazi la kibiashara na kusisitiza kwamba Serikali itaendelea kuziwezesha Taasisi zake kuwa na miradi mikubwa itakayoziwezesha kujitegemea.
 
Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa jengo la makazi la kibiashara lililo sekei jijini Arusha Dkt. Mpango amesema Serikali imeiruhusu Wakala wa Majengo Nchini (TBA) kushirkiana na sekta binafsi kwa ubia ili kuiwezesha kutekekeza miradi ya kimkakati na itakayoleta tija haraka na hivyo kupunguza utegemezi wake kwa Serikali.
 
“Nawapongeza kwa ujenzi wa jengo zuri la kisasa, endeleeni na mpango wa kujenga majengo ya aina hii katika maeneo mbalimbali ya kimkakati yatakyowezesha kuhudumia kaya nyingi na zingatieni uhifadhi wa mazingira na kwa kupanda miti na maua na kuweka mifumo mizuri ya kuondosha takataka’ amesema Dkt. Mpango.
 
Dkt. Mpango ameitaka TBA kufanya uwekezaji wenye tija katika maeneo yake na kuhakikisha wapangaji wa majengo yake wanalipa kodi kwa wakati.
Ameitaka Wizara ya Uwekezaji kuhakikisha inaweka msukumo kwenye ujenzi wa viwanda vya vifaa vya ujenzi ili kupunguza gharama za ujenzi hivyo kuwezesha Serikali kufikia lengo la ujenzi wa nyumba nyingi zitakazokidhi mahitaji ya ongezeko la idadi ya watu.
 
“Serikali imedhamiria kukuza sekta ya nyumba ili ichangie pato la Taif ana hivyo kukuza uchumi’ amesisitiza Dkt. Mpango.
 
Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema kuwa azma ya ujenzi huu ni chimbuko la TBA la kutaka kujiendesha  kibiashara na hivyo kupata faida.
 
"Mfumo wa kisaa wa vitasa janja ili kudhibiti wapangaji wenye madeni na hivyo kusaidia ulipaji wa kodi kwa muda muafaka, lengo ni TBA ni kupata mapato zaidi na kujiendesha yenyewe." amesisitiza Prof. Mbarawa.
 
Naye Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula, ameipongeza TBA kwa kujenga majengo marefu yanayohudumia idadi kubwa ya watu na kusisitiza kuwa majengo hayo yaendane na uwepo na maegesho ya magari.
 
Amesisitiza kuwa mahitaji ya nyumba nchini zaidi ya 390,981 kwa mwaka wakati nyumba zinazojengwa na taasisi mbalimbali kwa mwaka ni chini ya 2,000.
 
Amewataka wadau mbalimbali wa ujenzi waendelee kujenga nyumba ili kuendana na ongezeko la idadi ya watu ambapo inakadiriwa takriban watu zaidi ya milioni 1.6 wanaongezeka kila mwaka.
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela amesema jengo hilo lenye sakafu 11 limeongeza thamani ya mji wa Arusha hususan kipindi hiki ambacho idadi ya watalii imeongeza na hivyo kuchochea shughuli za biashara katikati ya jiji.
 
Awali akitoa taarifa ya mradi huo, Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Daud Kondoro amesema kukamilika kwa mradi huo utawezesha Wakala kujenga majengo mengine marefu ya makazi na biashara katika eneo la Sekei ili kuhamasisha shughuli za Utalii katika jiji hilo.
 
"Tumejipanga kuhakikisha miradi ya makazi na biashara iliyoko Canadian - Masaki, jijini Dar es Salaam, Ghana Kotta jijini Mwanza, Tameke Kotta na nyumba 150 (Awamu ya Pili) eneo la Nzunguni  jijini Dodoma inakamilika ili kuiwezesha TBA kuondokana na utegemezi kwa Serikali’ amefafanua Arch. Kondoro.
 
Jengo la makazi la kibiashara eneo la Sekei lenye sakafu 11 lina uwezo wa  kuhudumia kaya 22 na limegharimu zaidi ya shilingi bilioni 6.8 ambapo ujenzi wake umetekelezwa katika awamu nne.
Posted by MROKI On Friday, August 04, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo