Nafasi Ya Matangazo

August 05, 2023

Na Mwandishi wetu
Zoezi la wanaojiandikisha kuhama kwa hiyari hifadhini Ngorongoro limechukua sura mpya baada ya kuibuka kwa kundi jipya lenye mtazamo tofauti linalotaka kuruhusiwa kuhamia wanakotaka wenyewe kwa sharti tu la Serikali kuwalipa fidia zao na kuwahamisha.

Baadhi ya wakazi wa vijiji kadhaa wenye mtazamo huo wanasema wao wapo kila sehemu Tanzania nakwamba ni vyema Serikali ikatoa uhuru huo wa wao kwenda wanakotaka.

Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Erkepusi Mbokieni Sapuo anasema yeye na familia yake wamechagua kwenda uelekeo wa Engaruka ambapo tayari kuna ndugu zao wengine wanaishi huko muda mrefu.

"Tunaomba turuhusiwe kuhamia popote nje ya Ngorongoro bila ya kwenda Msomera."

"Tunaiomba Serikali itupe fidia sisi tunataka kuhama lakini sio lazima twende kulikopangwa na Serikali."

"Pawe na uhuru wa mtu kuchagua kama anataka kwenda Msomera sawa, kama anataka kwenda Kitwai sawa na kama hataki kwenda kokote kati ya huko sawa".

"Mimi nataka niende maeneo ya Engaruka, Serikali inifidie niende na ndugu zangu." Amesema Sepuo

Itakumbukwa kwamba tayari kaya zaidi ya 500 zimehama kwa hiyari kuelekea Msomera, Handeni mkoani Tanga na Serikali imetangaza kuanza kwa mchakato wa ujenzi wa nyumba nyingine 5000 katika maeneo ya Msomera, kilindi na Kitwai Kwa ajili ya kuwahakikishia wakazi wa Ngorongoro wanaoendelea kujiandikisha Kwa hiyari.

Kuibuka kwa kundi hili linalotaka kuhamia mahala wanapotaka wenyewe ni mwendelezo wa kueleweka kwa zoezi hilo muhimu kwa UHIFADHI na Ustawi wa maisha yao.

Posted by MROKI On Saturday, August 05, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo