Wananchi wa Halmashauri ya Chalinze, Mkoani Pwani wametakiwa kuondoka tofauti zao Ili waweze kufikia mafanikio ya maendeleo.
Ushauri huo umetolewa leo na Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Ndg. Ridhiwani kikwete akizungumza na wananchi wa kata ya Bwilingu na Ubena kwa nyakati tofauti akiwasisitiza kuyakimbilia maendeleo.
Mbunge huyo ameyasema baada ya ukaguzi wa miradi na kuongea na wananchi baada ya ukaguzi. Katika ziara hiyo Ndugu Mbunge Kikwete amezindua program ya ukusanyaji taka yenye lengo la kutengeneza mazingira na kufanya Mji wa Chalinze kuwa msafi na baadae kukagua ujenzi wa Mabweni, Zahanati kabla ya kuzungumza na wananchi katika kijiji cha Ubena zomozi na baadae Lulenge katika kijiji cha Kaloleni mjini hapo.
0 comments:
Post a Comment