Nafasi Ya Matangazo

July 11, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa Taasisi mbalimbali, Wanafunzi pamoja na Wananchi wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika yaliyofanyika katika ukumbi wa Nyasa uliopo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha tarehe 11 Julai, 2023.
***********
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema moja ya vikwazo vikubwa vya maendeleo barani Afrika ni pamoja na janga la rushwa ambalo linadhoofisha mifumo ya kitaasisi na kuathiri mipango na mikakati ya kujikomboa kiuchumi.
 
Rais Samia amesema hayo leo wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika na maadhimisho ya utekelezaji wa miaka 20 ya Mkataba wa Umoja wa Afrika wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa yaliyofanyika AICC.
 
Aidha, Rais Samia amesema viongozi wote barani Afrika hawana budi kuimarisha ushirikiano katika mapambano dhidi ya rushwa.
 
Vile vile, Rais Samia amewataka viongozi kutafakari na kuchambua kwa dhati masuala ya rushwa ili kubainisha changamoto au vikwazo vya mapambano hayo na kuchukua hatua muafaka.
 
Kwa upande mwingine, Rais Samia amesema Serikali inaendelea kuimarisha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kibajeti na kimfumo ikiwemo kuanzisha taasisi zinazosimamia utawala bora na haki za binadamu nchini.
 
Rais Samia pia amesema Serikali imewekeza zaidi katika matumizi ya mifumo ya TEHAMA inayosaidia kupunguza mawasiliano ya ana kwa ana katika kutoa huduma kama michakato ya zabuni, usajili wa biashara na namba ya mlipa kodi ili kupunguza mianya ya rushwa.  
 
Kupitia Divisheni ya Mahakama Kuu inayosikiliza kesi za washtakiwa wa makosa ya rushwa kubwa, Serikali imeokoa na kudhibiti matumizi ya fedha yasiyostahili ya zaidi ya Shilingi bilioni 139 kuanzia mwaka wa fedha 2019/20 hadi 2021/22.

Viongozi wa Dini, Maafisa kutoka Taasisi mbalimbali, Wanafunzi pamoja na Wananchi wakiwa kwenye ukumbi wa Nyasa uliopo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha kwa ajili ya Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika tarehe 11 Julai, 2023.

Viongozi wa Dini, Maafisa kutoka Taasisi mbalimbali, Wanafunzi pamoja na Wananchi wakiwa kwenye ukumbi wa Nyasa uliopo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha kwa ajili ya Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika tarehe 11 Julai, 2023.

Posted by MROKI On Tuesday, July 11, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo