Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Kigoma Ujiji Bi. Mwantum Mgonja ameipongeza kampuni ya Mainstream
Media Limited kwa uwekezaji mkubwa uliofanywa katika mkoa wa Kigoma.
Pongezi hizo zimetolewa mbaada
yakampuni hiyo kuanzisha kituo che redio
cha Main Fm 91.7 ambayo kutoa habari na taarifa katika mambo mbalimbali ya
kimaendeleo yanayofanywa na serikali ndani ya mkoa wa Kigoma
Bi. Mwantum ameyasema hayo wakati
wa mahojiano katika studio za Main Fm kwenye tukio la kuwasha kipaza sauti (mic)
kwa mara ya kwanza.
Mkurugenzi huyo alisema serikali
imetoa fedha kwa ajili ya kujenga na
kuboresha miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya manispaa ya Kigoma Ujiji
katika sekta mbalimbali hususani afya na elimu
na pia ni bahati na kusema redio
hiyo itasaidia kutoa taarifa za aina hiyio kwa umma huku akishukuru kwa kupata
fursa ya kukizindua.
Aidha mkurugenzi huyo pia alipata
fursa ya kutoa ufafanuzi juu ya mambo mbali mbali ambapo alisema kuwa mfuko wa
maendeleo ya vijana unafanyiwa marekebisho na kuwataka vijana wa Mkoa wa Kigoma
kuendelee kusikiliza vyombo vya habari hususani Main fm 91.7 kwa ajili ya kujua
fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya mkoa wa Kigoma ikiwemo mikopo nafuu
inayotolewa na serikali kwa ajili ya kuwainua vijana kiuchumi.
Mwantum aliambatana na diwani
viti maalum kata ya Mwanga Kusini,mtendaji wa kata ya Mwanga Kusini na
mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa kilimahewa pamoja na wadau mbalimbali kutoka ndani ya mkoa wa Kigoma.
Zoezi hili ya Kuwasha Vipaaza sauti
(Mic) kwa mara ya kwanza lilifanyika Tarehe 10 Julai 2023.
Mainstream Media Limited, pamoja
na uwekezaji huo pia wametoa fursa za ajira kwa Watangazaji na wadau wa tasnia
ya habari kutoka maeneo mbali mbali
duniani ili kuhakikisha kuwa kituo chao hicho kinafikisha ujumbe kwa urahisi na
haraka zaidi kote duniani.
Zoezi la kuwasha Vipaaza sauti
(Mic) lilienda sambamba na kuwaruhusu wasikilizaji wa redio hii duniani kote
kuisikiliza kupitia kwenye tovuto ya Main FM (www.mainfm.co.tz)
Pia Meneja wa kituo Bw. Felician
hulilo, alisema kuwa RMain FM imeanzia Kigoma lakini menejimenti yake imelenga
kuipeleka katika mikoa yote ya Tanzania.
0 comments:
Post a Comment