Waziri wa maji Juma Aweso
akiongea na wananchi wa wilaya ya kaliua mkoani Tabora wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi wa mradi wa maji wa miji 28
.
Waziri wa maji Juma Aweso
akimtwisha ndoo ya maji mama huyo katika hafla fupi baada ya kuweka jiwe la
msingi. .
Wanaonekana kwenye picha
wakiwa na Waziri wa maji Juma Aweso ni wakanadarasi wataotekeleza mradi wa maji
kutoka ziwa Victoria kupeka katika wilaya za Kaliua Sikonge na Urambo.
Katibu Tawala wa mkoa wa Tabora Dkt
John Mboya akizungumza mbele ya waziri wa maji Juma Aweso.
Na Lucas Raphael,TaboraWaziri wa maji Juma Aweso
amesema wizara inatekeleza miradi mbalimbali ya maji nchini ili kufikia malengo
yaliyowekwa na Ilani ya ccm Ifikapo mwaka 2025 upatikanaji wa maji mijini uwe
asilimia 95 na vijijini uwe asalimia 85.
Alitoa kauli hiyo kwenye uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa maji wa miji wa 28 unaotekelezwa na wizara ya maji uliofanyika katika wilaya ya kaliua mkoani Tabora .
Aweso alisema kwamba upatikanaji wa maji katika wilaya ya kaliua siyo wa kuridhisha ,kwani mahitaji ya maji kwa sasa ni wastani ni lita 16,961,175 kwa siku .
Alisema kwamba kwa sasa wilaya hiyo inapata maji chini ya wastani huo ambapo kwa sasa maji yanayopatina ni lita 7,971,423 kwa siku na hivyo kufanya kaliua kuwa na upungufu wa lita 8,989,423 kwa siku.
Waziri huyo wa maji alisema kwamba mji wa kaliua mahitaji yake kwa siku ni lita 1,535,150 ,wakati uzalishaji ni lita 675,466 na hivyo kuwepo na upungufu wa lita 859,684 na kufanya hali ya upatikanaji wa mji mjini kuwa asilimia 44.
Aweso akiongelea upande wa maji vijiji alisema mahitaji ni lita 15,426,025 kwa siku ila maji yanayozalishwa ni lita 7,250,232 na kuwa na upungufu wa lita 8,175,793 na kufanya hali ya upatikanaji wa maji vijijini kufikia asilimia 49.
Waziri Aweso akiongelea mradi wa maji kutoka ziwa Victaria kutoka Tabora kwenda wilaya za Kaliua, Sikonge na Urambo unaotekelezwa na kampuni ya Megha Infrastructure Company Limited kutoa India mradi utakamilika mwaka 2025 utakaogharimu kiasi cha shilingi billion 143.26.
Hata hivyo aliwataka wataaluma wa Tuwasa wanaotekeleza mradi huo kuhakikisha mradi huo unakamilika mwezi Agasti mwaka huu ili wananchi waweze kupata huduma ya maji safi na salama
Awali mkurungezi wa mamlaka ya maji na usafi wa mazingira TUWASA Mayunga Kashilim alimweleza waziri wa maji Juma Aweso kwamba kukalika kwa mradi huo wa maji wananchi wapata 3700 watanufaika na umegarimu kiasi cha shilingi milioni 503 .
0 comments:
Post a Comment