Muonekano wa barabara ya Mto
wa Mbu - Loliondo sehemu ya Waso –Sale KM 49 wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Akizungumza wakati
akifungua rasmi barabara ya Mto wa Mbu -
Loliondo sehemu ya Waso –Sale KM 49 ,
Dakta, Mpango amesema nia ya Serikali ni kuijenga na kuikamilisha barabara yote
lakini kwa hatua ya sasa ni vema ikajengwa sehemu ya tatu mara baada ya kukamilika
kwa sehemu ya kwanza.
“Najua kuwa
mmeshaisanifu barabara yote toka Mto wa Mbu hadi Loliondo KM 217, sasa baada ya
kumaliza sehemu ya kwanza ya Waso-Sale KM 49, hamieni sehemu ya tatu ya
Ngaresero - Engaruka KM 39.2 kwa kuwa sehemu hiyo ina changamoto nyingi kwa
wasafiri na wasafirishaji”, amesema Dakta, Mpango.
Ameitaka Wizara ya
Ujenzi na Uchukuzi kuhakikisha barabara kuu na za mikoa zinapitika wakati wote
wa mwaka na kuwataka wananchi kuzitunza na kuzilinda ili zidumu kwa muda mrefu
na kuleta tija kwa wafugaji, wakulima, wafanyabiashara na watalii na hivyo kuchochea maendeleo.
Naibu Waziri wa Ujenzi
Eng. Godfrey Kasekenya amesema Wizara itaendelea kuhakikisha inafanya
matengenezo maalum ili sehemu ya pili ya Sale-Ngaresero KM 57.4 na sehemu ya
nne ya Engaruka- Mto wa Mbu KM 60.9 nazo ziwe katika ubora na kupitika wakati
wote wa mwaka.
Aidha amesema Wakala wa
Barabara nchini (TANROADS), umepanga kujenga kwa kiwango cha lami sehemu ya Waso-Loliondo
KM 10 ili kuunganisha na kuupendezesha
mji wa Loliondo.
Mtendaji Mkuu wa
TANROADS Eng. Rogatus Mativila amesema
barabara ya Waso –Sale KM 49 imejengwa na mkandarasi China Wu Yi Co. Ltd kwa zaidi ya shilingi
bilioni 87 na kukamilika kwake kutachochea ustawi wa sekta nyingine za kiuchumi
hususan utalii,kilimo na ufugaji.






0 comments:
Post a Comment