Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa, akisisitiza jambo wakati akikagua hatua za utekelezaji wa mradi wa ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Mianzini - Olemringa - Ngaramtoni Juu na Olemringaringa - Sambasha – Timbolo (Km 18) ambao ujenzi wake umefikia asilimia 23, mkoani Arusha. Kushoto ni Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo.
Meneja wa Wakala wa Barabara
Nchini (TANROADS) Mkoa wa Arusha, Eng. Reginald Massawe, akifafanua jambo kwa Waziri
wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa pamoja na uongozi wa mkoa wakati
wakikagua barabara ya Mianzini - Olemringa - Ngaramtoni Juu na Olemringaringa -
Sambasha – Timbolo (Km 18) kwa kiwango cha lami ambao ujenzi wake umefikia
asilimia 23, mkoani humo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Arusha, Steven Zelothe, akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof.
Makame Mbarawa, wakati Waziri huyo akikagua ujenzi wa barabara ya Mianzini - Olemringa - Ngaramtoni
Juu na Olemringaringa - Sambasha – Timbolo (Km 18) kwa kiwango cha lami mkoani
Arusha. Ujenzi wa barabara hiyo umefikia asilimia 23 na unatarajiwa kukamilika
mwezi Agosti, 2023.
Kazi za ujenzi wa barabara ya
Mianzini - Olemringa - Ngaramtoni Juu na Olemringaringa - Sambasha – Timbolo
(Km 18) kwa kiwango cha lami zikiendelea mkoani Arusha. Ujenzi wa barabara hiyo
umefikia asilimia 23 na unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti, 2023.
Serikali imeahidi kulipa fidia
kwa wananchi wa maeneo ya mianzini wanaopitiwa na ujenzi wa barabara ya
Olemringaringa - Ngaramtoni Juu yenye urefu wa kilometa 8.5 inayoendelea
kujengwa kwa kiwango cha lami.
Hayo yamesemwa jijini Arusha na
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, wakati alipokagua hatua za
utekelezaji wa mradi huo wenye jumla ya urefu wa kilometa 18 unaoanzia Mianzini
- Olemringa - Ngaramtoni Juu na Olemringaringa - Sambasha - Timbolo ambao
umefikia asilimia 23 ya utekelezeji wake.
“Sehemu ambazo barabara imefuata wananchi, tutawalipa mara baada ya zoezi la tathmini linaloendelea kukamilika kwani ni haki yao”, amesema Prof. Mbarawa.
Amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo ni ahadi iliyotolewa na Rais wa Awamu ya Tano, Hayati. Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kujengwa kwa kiwango cha lami na unafadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia mia moja na utatekelezwa kwa muda wa miezi 15 ambapo unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Agosti, 2023.
“Serikali hii ni sikivu na inaendelea kutekeleza ahadi zilizotolewa na Serikali za Awamu zilizopita ili kuendelea kuboresha hali ya miundombinu nchini na kufungua mawasiliano hususani katika miundombinu ya barabara”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa ametoa wito kwa Meneja wa Mkoa wa TANROADS kusimamia ujenzi wa barabara hiyo na kuhakikisha thamani ya fedha na ubora wa barabara unaonekana pale ujenzi utakapokamilika.
Naye, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Steven Zelothe, amempongeza Mhe. Rais wa Awamu ya Sita kwa kuwa wananchi wanaendelea kuona juhudi za dhati zinazoendelea kufanywa na Serikali hii hasa kwa mkoa wa Arusha.
Kwa upande wake, Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini, Mrisho Gambo amesema kuwa mradi huo utakapokamilika utarahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji wa haraka wa wakazi wa maeneo hayo na kuongeza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja.
Awali akitoa taarifa ya mradi, Meneja wa TANROADS mkoa wa Arusha Eng. Reginald Massawe, ameeleza kuwa barabara hiyo imesanifiwa kubeba ekseli za magari zipatazo milioni 3 zenye uzito wa tani 8 kila moja katika muda wa miaka 20.
Amesema kuwa hadi sasa mkandarasi amekwishaleta mitambo, vifaa na magari yanayotumika kwenye kazi za ujenzi wa barabara hiyo na matumaini yao mradi utakamilika kama ulivyopangwa.
Ujenzi wa wa barabara ya Mianzini – Olemringaringa – Ngaramtoni Juu na Olemringaringa - Sambasha/Timbolo (Km 18) unatekelezwa na mkandarasi kutoka kampuni ya STECOL Corporation kutoka China kwa gharama ya Shilingi Bilioni 22.226.
0 comments:
Post a Comment