Nafasi Ya Matangazo

March 30, 2023

Naibu waziri wa Nishati Stephen Byabato na viongozi waandamizi wa Tanesco wakifurahia baada ya uzinduzi wa mpango wa miaka minne wa masuala ya jinsia kwa shirika la umeme Tanzania TANESCO
Mkurugenzi wa TANESCO Maharage CHande (Kulia) akisalimiana na Naibu waziri Mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi.
Sehemu ya washiriki
Naibu waziri wa Nishati Stephen Byabato akikata utepe kuashiria uzinduzi wa programu ya miaka minne ya masuala ya jinsia
Na Neema Mbuja, DODOMA
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kushirikiana na Benki ya Dunia kupitia mradi wa kusafirisha umeme mkubwa kutoka Tanzania hadi Zambia (TAZA) imezindua mpango wa miaka minne wa masuala ya jinsia unaoanza kutekelezwa chini ya Benki ya dunia
Progamu hii imezinduliwa na Mgeni Rasmi na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Stephen Byabato ukiwa na lengo la kutatua changamoto wanazokutana nazo wafanyakazi wanawake katika maeneo yao ya kazi na kuongeza uwiano wa utendaji kazi baina ya wanawake na wanaume kati ya mwaka 2023 hadi 2026.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo, Mhe. Byabato alisema TANESCO imejizatiti kwa kiasi kikubwa kwenye usawa wa kijinsia na kuitaka menejimenti ya Shirika hilo kuhakikisha inaanzisha kitengo maalumu cha jinsia ili kuwepo na uwanja mpana wa kujadili masuala ya kijinsia.

"Naiagiza menejimenti ya TANESCO kupitia mradi wa TAZA kuhakikisha wanawake wanapewa kipaumbele sawa na wanaume na kuongeza fursa zaidi kwa wanafunzi wa vyuo ambao wanajiandaa kuajiriwa kwenye ajira rasmi".

Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Bw. Maharage Chande alisema kuwa Shirika tayari lilishaanza kutekeleza programu ya masuala ya jinsia, ila kupitia mradi wa TAZA masuala ya kijinsia yataongezwa kwenye sera na taratibu za Shirika.

Ameyataja maeneo ya kipaumbele kuwa ni pamoja na sera ya Shirika kutoa kipaumbele kwenye masuala ya jinsia, upatikanaji wa taarifa sahihi za masuala ya jinsia kwenye taasisi na kuwepo kwa nafasi za mafunzo ya ukuzaji taaluma kwa wafanyakazi wanawake hasa wanaofanya kazi za kiufundi ili kuwajengea uwezo kupitia mpango wa mafunzo kazini.

Mradi wa TAZA unatekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kupitia mkopo wa Jumuiya ya  Maendeleo ya Kimataifa (IDA) ya Benki ya Dunia, mkopo wa Mfuko wa Maendeleo wa Ufaransa (AfD), Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Posted by MROKI On Thursday, March 30, 2023 No comments
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Mary Masanja akigawa mitungi ya gesi 100 kwa wanawake wajasiriamali.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Mary Masanja amegawa vifaa vya Michezo mashuleni Mkoani Mwanza.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Mary Masanja amegawa vifaa vya Michezo mashuleni Mkoani Mwanza.
Picha ya pamoja.


Vifaa hivyo vya michezo vilivyokabidhiwa kwa shule za Sekondari za Nansio, Bukongo na Namagondo ni pamoja na mipira na jezi vyenye thamani ya shilingi milioni 3,350,000.

Pia katika ziara hiyo, Mhe. Masanja amekabidhi fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 3,000,000 kwa ajili ya kuwasaidia wajasiriamali hao kuendelea kujinunulia nishati gesi kwa ajili ya biashara zao.

Awali akizungumza na wanafunzi hao, Mhe. Masanja aliwaasa kusoma kwa bidii,kuwa na hofu ya Mungu , nidhamu na kuwaonya kutojihusisha na mambo ambayo sio utamaduni wa Mtanzania.

Aidha aliwataka wajasiriamali  kutumia nishati mbadala na kuachana na matumizi ya nishati chafu ambayo ina athari kwa afya ya binadamu na mazingira kwa ujumla.
Posted by MROKI On Thursday, March 30, 2023 No comments
Balozi wa Tanzania nchini Sudan kusini Balozi John Simbachawene kushoto akimpongeza Bw. Benson Meikoki Meneja Mauzo na Masoko Kiwanda cha madawa cha Kairuki (KPIL) mara baada ya kuwasilisha mada Katika kongamano la msafara wa kibiashara wa Tanzania uliotembelea nchini Sudan Kusini Katika jiji la Juba ili kuang mialia fursa mbalimbali za kibiashara na uwekezaji Katika sekta ya Kilimo afya na Elimu.
Bw. Benson Meikoki Meneja Mauzo na Masoko Kiwanda cha madawa cha Kairuki (KPIL) kilichopo chini ya mtandao wa mashirika ya Kairuki (KHEN) akiwasilisha mada Katika kongamano la msafara wa kibiashara wa Tanzania uliotembelea nchini Sudan Kusini Katika jiji la Juba ili kuangalia fursa mbalimbali za kibiashara na uwekezaji Katika sekta ya Kilimo afya na Elimu.
Balozi wa Tanzania nchini Sudan kusini Balozi John Simbachawene akiwa Katika picha ya pamoja na Bw. Benson Meikoki Meneja Mauzo na Masoko Kiwanda cha madawa cha Kairuki (KPIL) mara baada ya kuwasilisha mada Katika kongamano la msafara wa kibiashara wa Tanzania uliotembelea nchini Sudan Kusini Katika jiji la Juba ili kuangalia fursa mbalimbali kibiashara na uwekezaji Katika sekta ya Kilimo afya na Elimu.
Picha ya pamoja
Picha mbalimbali zikionesha Washiriki wa kongamano Hilo waliokuwemo Katika msafara huo wa kibiashara ulioandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TANTRADE.
*****""******"
Meneja Mauzo na Masoko Kiwanda Cha Madawa Cha Kairuki Pharmaceutical industry LTD(KPIL) Bw. Benson Meikoki amesema wataendelea kushirikiana na nchi mbalimbali Afrika Kwa kuwapatia Maji tiba (Drips) na Dawa za maji wanazozitengeneza katika Kiwanda hicho Ili kuendelea kutanua wigo wa sekta ya Afya katika Mataifa hayo.

Meikoki ameeleza hayo jijini Dar es salaam wakati wa majumuisho ya safari yao, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu safari yao ya kibiashara ambayo wamefanya nchini Sudan Kusini ambayo iliandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Baishara Tanzania TANTRADE

Amesema Kiwanda hicho kilipata fursa ya kushiriki msafara wa kibiashara baina ya nchi ya Tanzania na Sudan Kusini ambapo walikuwa na wadau wa sekta ya Afya, Kilimo na Elimu na wajasiriamali Ili kujadili namna gani Tanzania itaweza kushirikiana na nchi ya Sudan Kusini katika sekta hizo.

Amesema Kiwanda Cha Madawa cha Kairuki(KPIL) ndio kilipewa dhamana ya kunadi sera zake kama mwakilishi wa Viwanda vya madawa Tanzania ambapo alielezea Masuala mbalimbali , awali alielezea Mtandao wa mashirika ya Kairuki (KHEN) ikiwa ni pamoja na Hospitali ya Kairuki ambayo imekuwa ikiendelea kuwa Hospitali bora nchini toka mwaka 1987.

Aidha amesema katika Hospitali hiyo imekuwa na mafanikio makubwa kwani pia wamefungua kituo cha Upandikizaji Mimba (Kairuki IVF) kilichopo Bunju mazizini Ili kuweza kurahisisha huduma hiyo kupitia Wataalamu waliobobea kama vile Dkt. Clementina Kairuki na hivyo kuepusha gharama za safari za kwenda nje ya nchi kutafuta huduma hiyo.

“Kupitia Mkutano huu tuliweza kueleza kuwa kwa sasa Afrika haiwezekani kutokuwa na mtoto bali anapatikana KAIRUKI IVF alisema Meikoki, pamoja na mambo mengine alisema mtandao huo wa KHEN una chuo kikuu cha madaktari , na chuo cha manesi.

Meneja Huyo ameendelea kusema Kiwanda Cha Kairuki kimeweza kutengeneza na kuzalisha chupa Mill 60 Kwa Mwaka lakini pia kuajiri wafanyakazi zaidi ya 500.

Amesema miongoni mwa madawa mbalimbali ambayo yanazalishwa katika Kiwanda hicho ni pamoja Ringer Lactate,Mannitol, Paracetamol,Fluconazole,Ciprofloxacin,Sodium chloride 3% , DNS, NS, D5, D10, D50, na Nyingine nyingi.

Amesema pia wanafanya Biashara na wadau mbalimbali zikiwemo za ndani kama vile Msd Tanzania bara, CMS zanzibar visiwani, na mahospitali kama vile Muhimbili, Lugalo,Rabininsia, TMJ na nyingine nyingi na biashara za Nje kama vile Malawi,Zambia,Msumbiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Yemen,pamoja na nchi nyingine ambazo wapo kwenye hatua za mwisho za makubaliano.

Aidha ameeleza lengo na madhumuni ya Kiwanda hicho ni kuweza kuzihudumia nchi za SADC kwani katika safari hiyo wamefanya mazungumzo na Sudan kusini Ili kuangalia uwezekanao wa kufanya biashara na kupeleka madawa katika nchi hiyo.

Posted by MROKI On Thursday, March 30, 2023 No comments

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Daniel Chongolo akizungumza kwenye Kikao Kazi cha 18 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano kutoka Serikalini (TAGCO) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam Machi 29, 2023. Kikao hicho cha siku tano kimebeba kauli mbiu isemayo "Mawasiliano ya Kimkakati Injini ya Maendeleo". (PICHA NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID).


Katibu wa TAGCO, Bw. Abdul Njaidi (wapili kulia) na baadhi ya wajumbe wengine wa Kamati ya Utendaji ya TAGCO, wakisikiliza hotuba ya Ndg. Chongolo.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye, akizunhuzma kwenye Kikao hicho.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye, akizungumza kwenye Kikao hicho.
Mwenyekiti wa TAGCO, Bi. Sarah Kibonde
Washiriki wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Daniel Chongolo ( hayupo pichani).
Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Daniel Chongolo (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye.
Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Daniel Chongolo (katikati) na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Selestine Kakele. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Selestine Kakele akizungumza wakati wa kikao hicho.



Wajumbe wa Kamati Tendaji ya TAGCO
 Wajumbe wa TAGCO 
Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Daniel Chongolo (katikati) akisindikizwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa mara baada ya kuhutubia kikao kazi cha 18 cha TAGCO.

Posted by MROKI On Thursday, March 30, 2023 No comments
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Watumishi Housing Company Dr. Fred Msemwa (kulia) wakati alipotembelea mradi wa WHI Magomeni, Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Watumishi Housing Company Dr. Fred Msemwa akizungumza.
Watumishi wa WHI wakisikiliza 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ameielekeza Menejimenti ya Watumishi Housing Investments (WHI) kujenga nyumba za watumishi kwenye maeneo yenye fursa na mazingira mazuri ya kuishi ili kuwawezesha watumishi wote hata walio kwenye maeneo ya pembezoni kupata makazi bora ya kuishi yatakayowawezesha kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Mhe. Kikwete ametoa maelekezo hayo leo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kujitambulisha na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa Watumishi Housing Investments jijini Dar es Salaam.

Mhe. Kikwete amesema pamoja na kazi nzuri iliyofanywa na inayoendelea kufanywa na Watumishi Housing Investments, ni vizuri zaidi wakafikiria kujenga nyumba nyingi zaidi maeneo yenye uhitaji mkubwa wa nyumba hizo, akitolea mfano wa maeneo ya pembezoni mwa nchi ambayo ndio yenye uhitaji mkubwa wa nyumba.

“Mnafanya kazi nzuri sana ya ujenzi wa nyumba hizi, lakini mnatakiwa kuangalia fursa, maeneo gani yana uhitaji mkubwa wa nyumba, hasa maeneo ya pembezoni ili hata wanaohamishiwa huko wafurahie maisha na kutekeleza kikamilifu jukumu la kutoa huduma bora kwa wananchi,” Mhe. Kikwete amesisitiza.

Mhe. Kikwete ameongeza kuwa, pamoja na haki na stahiki nyingine wanazopata watumishi, mazingira mazuri ya kuishi ni jambo lingine la msingi ambalo linapaswa kupewa kipaumbele na WHI wakati wa utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa nyumba za kuishi watumishi wa umma.

Mhe. Kikwete amesema ni matarajio ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuona watumishi wa umma wanafanya kazi kwa bidii na maarifa, hivyo katika kufikia malengo ya Mhe. Rais, Watumishi Housing Investments wana nafasi kubwa ya kuunga mkono lengo hilo la Mheshimiwa Rais kwa kujenga nyumba bora kwa ajili ya kuziuza na kuwapangisha watumishi wa umma nchini.

“Taasisi zinazojenga nyumba ziko nyingi, wengine wanajikita kwenye ujenzi wa nyumba kwa ajili ya mwananchi yeyote lakini sisi Watumishi Housing Investments tuna malengo yetu ambayo yamejikita kwa watumishi wa umma
Posted by MROKI On Thursday, March 30, 2023 No comments

March 29, 2023

Katibu Mkuu wa Klabu ya Michezo ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Bw. Mbura Tenga (kulia), akimkabidhi kombe la ushindi wa jumla , Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA) walilolipata kutoka kwenye michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI), pia michezo ya Mei Mosi na mabonanza.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania, Bw. Mussa Mbura (wa kwanza kushoto) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Klabu ya Michezo ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Utamaduni), Bw. Mbura Tenga (kulia), akitoa historia fupi ya klabu hiyo, kwenye hafla ya kukabidhiwa vikombe vya ushindi wa michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za serikali (SHIMIWI), Mei Mosi na mabonanza.
Baadhi ya wanamichezo wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Bw. Mussa Mbura (watano kutoka kulia), baada ya kukabidhi vikombe vya ushindi wa michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI), Michezo ya Mei Mosi na bonanza.
**********
Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), imesema inathamini michezo mahala pa kazi na itaendelea kuwaruhusu watumishi wake kushiriki kwenye michezo mbalimbali inayoandaliwa na mashirikisho yanayotambuliwa.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Bw. Mussa Mbura alipokuwa akipokea vikombe zaidi ya 10 vya ushindi wa michezo ya mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI),  michezo ya Mei Mosi iliyofanyika mwaka 2022 mkoani Morogoro na Dodoma na bonanza lililofanyika kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Bw. Mbura amesema TAA inathamini michezo kwa kuwa inawaweka watumishi wake katika afya njema ya mwili na akili, ambapo husaidia huongeza ufanisi wa majukumu yao ya kazi.

“TAA tunaahidi kutoa ushirikiano mkubwa kwa kuendelea kutoa wachezaji wengi kama sasa wanaounda timu yetu ya Sekta ya Uchukuzi, inayoshiriki kwenye michezo mbalimbali, sote tunajua michezo ni afya, upendo na inajenga mahusiano na watu wengine na inajenga afya ya mwili na akili vinakaa vizuri, kwa hiyo muendelee kushiriki na msiache kutimiza majukumu yenu,” amesema Bw. Mbura.

Pia amesema pamoja na klabu hiyo kuwa na kupewa kipaumbele na menejimenti yote, bado TAA wamepokea maelekezo ya Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Bw, Gabriel Migire kwa watumishi kushiriki kwenye michezo, ili waendelea kuleta vikombe zaidi na kuheshimisha Wizara na hata kuongeza ufanisi na tija makazini.

Hatahivyo, ameahidi kuongeza bajeti ya michezo na kununua vifaa stahiki, ambavyo TAA watapangiwa na Wizara kununua kwa ajili ya michezo mbalimbali, ikiwemo baiskeli zitakazotumika kwenye mashindano.
Halikadhalika, ameahidi kutembelea kambi ya Klabu ya Sekta ya Uchukuzi, itakayoshiriki kwenye michezo ya Mei Mosi itakayoanza tarehe 14 hadi 29 April, 2023 mkoani Morogoro.

Awali Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Bw. Mbura Tenga ameishukuru TAA kwa ushirikiano wao mkubwa wa kutoa wachezaji wengi wanaoshiriki kwenye michezo mbalimbali.

“TAA mmekuwa mfano wa kuigwa kwa kutoa wachezaji wengi wenye vipaji ambao wamekuwa chachu ya kuleta ushindi kwenye klabu yetu ikiwa ni moja ya taasisi kubwa tano kati ya 14 zinazounda Sekta ya Uchukuzi, ambapo wapo wachezaji wanaocheza mchezo ya mtu mmoja mmoja na pia kama timu ambayo inatuletea makombe mengi, pamoja na kombe na ushindi wa jumla, hivyo tunawapongeza sana” amesema Bw. Tenga.

Bw. Tenga amesema Uchukuzi inatarajia kushiriki kwenye michezo ya soka, netiboli, kamba, riadha, kuendesha baiskeli, karata, bao, draft na mpira wa wavu.
Posted by MROKI On Wednesday, March 29, 2023 No comments

March 28, 2023

Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally  (katikati) akiwa ameambatana na Kaimu Sheikh wa Dar es salaam, Sheikh Walid Alhad Omar, wakiongozana na Mwenyeji wako, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRD, Abdulmajid Nsekela (kulia) wakati walipowasili kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja wake, wadau, pamoja na vituo vya watoto yatima, iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na zaidi ya watu 1,000. Picha zote na Othman Michuzi.
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally (watano kulia) kwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRD, Abdulmajid Nsekela (watatu kulia) wakikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula na mahitaji mengine kwa watoto wawakilishi wa moja ya kituo cha kuwalea watoto yatima, wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja wake, wadau, pamoja na vituo vya watoto yatima, iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam. Wapili kushoto ni Mkuu wa  Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo.
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally akizungumza na wageni mbalimbali walioalikwa katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja wake, wadau, pamoja na vituo vya watoto yatima, iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRD, Abdulmajid Nsekela akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja, wadau, pamoja na vituo vya watoto yatima, iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya  CRDB, Dkt. Ally Hussein Laay akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja, wadau, pamoja na vituo vya watoto yatima, iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
Kaimu Sheikh wa Dar es salaam, Sheikh Walid Alhad Omar akizungumza na wageni mbalimbali walioalikwa katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja wake, wadau, pamoja na vituo vya watoto yatima, iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Kitengo cha CRDB Al-Baraq, Rashid Rashid akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja, wadau, pamoja na vituo vya watoto yatima, iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.













 

Posted by MROKI On Tuesday, March 28, 2023 No comments
  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo