Wafanyakazi wa taasisi ya kifedha ya Faidika wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kushiriki katika zoezi la kuchangia damu salama ikiwa ni kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja
Mkuu wa Kitengo cha Mauzo, Masoko na Mifumo wa taasisi ya kifedha ya Faidika, Bw. Asupya Bussi Nalingigwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi la kuchangia damu salama ikiwa sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.
Mkuu wa Kitengo cha Mauzo, Masoko na Mifumo, wa taasisi ya kifedha ya Faidika Bw. Asupya Bussi Nalingigwa akichangia damu.
Meneja wa masuala ya Bima wa taasisi ya kifedha ya Faidika Julius Ming’anya akichangia damu.
***********
Na Mwandishi wetu
Taasisi ya huduma za kifedha ya Faidika imeadhimisha wiki huduma kwa wateja duniani kwa kuchangia damu salama kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Zoezi hilo limewahusisha wafanyakazi wote wa Faidika waliopo makao makuu jijini Dar es Salaam na matawi yao ya mikoani.
Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya taasisi hiyo eneo la Morocco jijini Dar es salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo, Masoko na Mifumo, Bw. Asupya Bussi Nalingigwa alisema kuwa wanajisikia fahari kubwa kushiriki katika zoezi la kuchangia damu salama ambayo itatumika kwa ajili ya wagonjwa mbalimbali wenye uhitaji.
Bw Nalingigwa alisema kuwa taasisi ya Faidika inafanya kazi na jamii ambao ndiyo wateja wao wakubwa, hivyo ni wajibu wao kushiriki katika shughuli za kijamii.
“Faidika ni taasisi ambayo ina wateja wa aina zote na kufanikiwa kuwafikia wateja wengi. Ni wazi kuwa jamii ina kutana na changamoto mbalimbali ambazo zinahitaji msaada. Zoezi la kchangia damu ni moja ya shughuli kubwa sana kijamii, kwan kki damu tunayochangia inakwenda kusaidia wagonjwa wenye huhitaji.
Kwa kuona hivyo, tumeamua kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kwa kuendesha zoezi hili na limefanikiwa sana kwani wafanyakazi wote wamechangia damu salama,” alisema Bw Nalingigwa.
Aliongeza kuwa hata matawi yao ya mikoani, wameshiriki katika zoezi hili na kwao litakuwa endelevu.
“Sisi tumechangia damu kwa ajili ya hospitali ya Taifa ya Muhimbili, wenzetu wa mikoani wamefanya hivyo kwa kuchangia hospitali au vituo vya afya. Ni faraja kubwa sana,” alisema.
Alifafanua kuwa Taasisi ya Faidika imezidi kutanua wigo wa shughuli zake kwa kutoa mikopo ya aina mbalimbali kwa wafanyakazi wa serikali, sekta binafsi na wajasiliamali.
Alisema kuwa mpaka sasa wametumia jumla ya Sh bilioni 68 kukopesha wafanyabishara wadogo wadogo na wafanyakazi wa sekta tofauti.
Alisema kuwa wameboresha huduma zao kwa wateja kwa asilimia 100 ambapo mikopo hiyo inatolewa ndani ya saa 24 tena kwa kigitali na kwa masharti nafuu.
Alisema kuwa kwa vile wanaendesha shughuli zao kidigitali wameweza kuwahudumia wateja wengi na kufanikiwa kupata mikopo mbalimbali ambapo kwa wafanyakazi wa serikali wanaweza kukopa kuanzia sh100,000 mpaka milioni 70 na kwa wafanyabiashara wadigo wadogo wanaweza kukopa kuanzia sh50,000 mpaka sh 50 milioni.
“Faidika inaendelea kuwawezesha watanzania ili waweze kuboresha maisha katika sekta mbalimbali ikiwa pamoja na elimu, afya na kilimo,” alisema.
0 comments:
Post a Comment