Nafasi Ya Matangazo

July 04, 2022


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya kushuhudia utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha nne kutoka Tabora- Isaka km 165 katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Julai, 2022.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya utiaji Saini Mkataba wa mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR kipande cha kutoka Tabora hadi Isaka na Mkataba wa Mhandisi Mshauri kwa ajili ya kutoa mafunzo ya uendeshaji wa Reli ya Kisasa (SGR).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha nne kutoka Tabora- Isaka km 165 katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Julai, 2022. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa akisaini Mkataba pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Yapi Merkez Bw. Aslan Uzun.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia utiaji saini Mkataba wa Mhandisi Mshauri kwa ajili ya kutoa mafunzo ya uendeshaji wa Reli ya Kisasa (SGR). Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa akiweka saini pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa KORAIL Bw. Park Tae-hun kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya utiaji Saini Mkataba wa mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR kipande cha kutoka Tabora hadi Isaka na Mkataba wa Mhandisi Mshauri kwa ajili ya kutoa mafunzo ya uendeshaji wa Reli ya Kisasa (SGR).
**********
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshuhudia utiaji saini Mkataba wa ujenzi wa reli ya kisasa kwa kipande cha nne kutoka Tabora hadi Isaka.
 
Hafla ya utiaji saini iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam imehusisha mikataba miwili, mmoja ukiwa ni kati ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Yapi Merkez ya Uturuki.
 
Mkataba mwingine ni kati ya TRC na kampuni ya KORAIL ya Korea kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo ya uendeshaji wa reli ambapo ni matayarisho ya kuwajengea watanzania uwezo wa kuiendesha na kuisimamia wenyewe.
 
Vile vile, Rais Samia amesema ujenzi wa kipande cha reli hii chenye kilomita 165 utasaidia kuunganisha mikoa tisa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Simiyu, Shinyanga na Mwanza.
 
Kwa upande mwingine, ujenzi huu pia utaiunganisha Tanzania na nchi za Uganda, Burundi, Rwanda, DRC, na Sudan Kusini na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara.
 
Gharama za ujenzi wa kipande cha nne katika Mkataba huu ni shilingi Trilioni 2.092 na gharama za vipande vyote vitano kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza ni shilingi Trilioni 16.792.
Posted by MROKI On Monday, July 04, 2022 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo