Mbunge Mteule wa Jimbo la Ngorongoro, Mkoani Arusha, Emmanuel Lekishon Shangai akionesha hati ya ushindi wa Kiti hicho aliyokabidhiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) baada ya kuibuka mshindi.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ngorongoro, Dkt.Jumaa Mhina (kushoto) akikabidhi cheti cha ushindi wa Kiti cha Ubunge kwa Mbunge Mteule wa Jimbo la Ngorongoro, kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Emmanuel Lekishon Shangai baada ya kuibuka mshindi kwa kupata kura 62,017 Kati ya kura 62,528 zilizopigwa katika Uchaguzi Mdogo uliofanyika Desemba 11,2021.
Saimon Paul Ngilisho aliyekua mgombea Ubunge wa Jimbo hilo kwa Tiketi ya Chama Cha Demokrasia Makini akitoa neno kuhusu mchakato mzima wa Uchaguzi huo.Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Wilson Mahera akizungumza na kuwashukuru Wadau wote wa Uchaguzi kwa kufanikisha Uchaguzi katika Jimbo la Ngorongoro.
Johnson Mahuma wa Chama Cha ACT Wazalendo akizungumza na kuipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa namna ilivyosimamia na kuendesha Uchaguzi huo Mdogo.
************Emmanuel Lekishon Shangai wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ametangazwa mshindi katika uchaguzi mdogo wa Jimbo Ngorongoro kwa kupata kura 62,017 Kati ya kura halali 62,461.
Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo Dkt.Jumaa Mhina amemtangaza leo Jumapili Desemba 12, 2021 katika kituo cha majumuisho cha Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha.
Katika matokeo hayo, Shangai amefuatiwa na mgombea wa Chama Cha ACT Wazalendo, Johnson Mahuma Gagu, aliyepata kura 170 kati ya kura 62,528 zilizopigwa.
Mgombea mwingine katika uchaguzi huo Saimon Paul Ngilisho wa Demokrasia Makinialipata kura 105 na Mohamed Kitundu wa ADC alipata kura 63 huku Mwinyi Hamisi wa ADA TADEA akipata kura 30.
Johnson Mahuma wa Chama Cha ACT Wazalendo akizungumza na kuipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa namna ilivyosimamia na kuendesha Uchaguzi huo Mdogo.
Zubeir Mwinyi Hamisi aliyegombea kwa Chama Cha ADA TADEA akitoa neno baada ya mshindi kutangazwa ambapo alimtaka mshindi kutekeleza Yale aliyowaahidi Wananchi wakati wa kampeni.
Sehemu ya wasimamizi wa Uchaguzi na wafuasi wa vyama wakifuatilia utangazwaji wa matokeo.
Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt.Wilson Mahera (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Uchaguzi, Hamidu Mwanga.
Wagombea na viongozi wa vyama vya Siasa wakiwa ukumbini hapo.
Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt.Wilson Mahera (Kulia) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mwl. Raymond Mangwala.
************
Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo Dkt.Jumaa Mhina amemtangaza leo Jumapili Desemba 12, 2021 katika kituo cha majumuisho cha Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha.
Katika matokeo hayo, Shangai amefuatiwa na mgombea wa Chama Cha ACT Wazalendo, Johnson Mahuma Gagu, aliyepata kura 170 kati ya kura 62,528 zilizopigwa.
Mgombea mwingine katika uchaguzi huo Saimon Paul Ngilisho wa Demokrasia Makini
Aidha katika Uchaguzi huo ulikua na Wagombea kutoka Vyama vya Siasa 11 ambapo vyama vingine vilivyopata kura katika Uchaguzi huo Mdogo uliofanyika Desemba 11 ni Mary Moses Daud wa UPDP aliyepata kura 20 huku Wagombea wa Juma Feruziyson wa NRA na Amina Amir Mcheka wa NLD walipata kura 16 kila mmoja.
Mwita Makuru wa UDP alipata kura kumi huku Saimon Johnson wa SAU aliyepata kura tisa (9) na Frida Marko Nko wa UMD akipata kura tano (5).
Ngorongoro wamechagua Mbunge baada ya aliyekua Mbunge wa Jimbo hilo, William Ole Nasha kufariki dunia.






0 comments:
Post a Comment