Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Mohamed Mchengelwa akizindua Mfumo wa maombi ya kazi kupitia simu za kiganjani uliofanyika katika ukumbi wa Tume ya Uchaguzi jijini Dodoma.Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Mohamed Mchengelwa (wa katikati), Naibu Waziri ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi (wa pili kushoto), Katibu Mkuu Utumishi na Utawala Bora Dkt. Laurean Ndumbaro(wa kwanza kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bi.Sophia Kaduma (wa pili kulia) pamoja na Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Bw. Samweli Tanguye wakifuatilia kwa umakini mfumo wa maombi ya kazi kupitia simu za kiganjani kwenye screan za ukumbi.
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi akitoa hotuba yake mbele ya Mgeni Rasmi kwa kuelezea namna ambavyo mfumo utafanya kazi na kuwasaidia waombaji fursa za ajira nchini.
Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye ukumbi wa Tume ya Uchaguzi wakishuhudia uzinduzi wa " Ajira Portal Mobile App" jijini Dodoma
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Mohamed Mchengelwa (wa tatu kutoka kulia aliyekaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Bw. Xavier Daudi ( wa kwanza kulia aliyekaa) pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Sekretarieti ya Ajira mara baada ya kuzindua Ajira Portal Mobile App.
Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Mohamed Mchengelwa (wa tatu kutoka kulia aliyekaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu Waziri Mhe. Deogratius Ndejembi (wa pili kutoka kulia aliyekaa), Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Laurean Ndumbaro ( wa pili kutoka kushoto aliyekaa) Mwenyekiti wa Bodi ya Sekretarieti ya Ajira Bi.Sophia Kaduma (wa kwanza kushoto aliyekaa) na Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Bw. Xavier Daudi ( wa kwanza kulia aliyekaa) pamoja na wawakilishi kutoka Mradi wa Maendeleo PS3+ mara baada ya kuzindua Ajira Portal Mobile App.
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Mohamed Mchengelwa (wa tatu kutoka kulia aliyekaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Menejimenti ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma mara baada ya kuzindua Ajira Portal Mobile App.
***********
Sekretarieti
ya Ajira katika Utumishi wa Umma imezindua App ijulikanayo kama “Ajira Portal
Mobile App” ambayo itakuwa na manufaa makubwa kwa waombaji fursa za ajira
kupata taarifa za uwepo wa nafasi za kazi, taarifa za nichakato ya ajira
kupitia simu zao za kiganjani.
Katibu
wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi
wa Umma Bw.Xavier Daudi amesema kuwa huduma hii itakuwa inapatikana kwenye
Playstore za simu janja na waombaji wa fursa za ajira wataweza kujisajili,
kuingia kwenye akaunti zao, kupakia taarifa za vyeti vyao na kuomba kazi
kupitia mobile app hiyo.
Aidha,amesema
kuwa uwepo wa huduma hii utaongeza wigo wa upashanaji wa habari na kuokoa fedha
zilizokuwa zikipelekwa kwenye internet café na baadhi ya waombaji fursa za
ajira. Pia amesema mfumo huu utasaidia upatikanaji wa taarifa za walioajiriwa
ndani ya sekta ya umma kuwa rahisi zaidi, kuwaondolea usumbufu waombaji wa
fursa za ajira kwa kutumia mfumo mmoja wa ajira na utapunguza siku za kuendesha
usaili kutoka siku 42 za sasa hadi kufikia siku 38.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.
Mohamed Mchengelwa (Mb) amesema kuwa ili Sekretarieti ya Ajira iweze kutekeleza kwa ufanishi majukumu yake inahitaji ushirikiano na
uwajibikaji wa mtu mmoja mmoja katika eneo lake ikiwemo waombaji wa fursa za
ajira Serikalini, Waajiri wa Taasisi za Umma na wadau mbalimbali wa maendeleo.
“Nayasema
mambo haya ili tuone suala la ajira katika Utumishi wa Umma ni suala la
msingi na muhimu linalotuwezesha kupata
nguvu kazi yenye ubunifu,ujuzi na maadili mema ili kuiwezesha Serikali
kutekeleza ipasavyo malengo yake inayojiwekea hususani kufikia Uchumi wa kati
wa Juu” alikaririwa akisema.
Hata
hivyo Waziri Mchengelwa ameipongeza Sekretarieti ya Ajira kwa ubunifu na maboresho
ambayo imekuwa ikiyafanya kwa kutumia TEHAMA ili kurahisisha utekelezaji wa
majukumu yao muhimu.
Waziri Mchengelwa alizindua” Ajira portal Mobile App “jijini Dodoma katika ukumbi wa Tume ya Uchaguzi hafla ambayo ilihudhuriwa na waombaji fursa za ajira katika Utumishi wa Umma, Wawakilishi kutoka Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma PS3, Wajumbe wa Bodi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma pamoja na Menejimenti ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
0 comments:
Post a Comment