Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selmeni Jafo akizungumza na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa ya Tanzania wakati wa mafunzo ya uongozi yaliyoandaliwa na Taasisi ya Uongozi leo Julai mosi, 2021 jijini Dodoma.
Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selmeni Jafo (hayupo pichani) wakati akizungumza kwenye mafunzo ya uongozi kwa viongozi hao. |
Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selmeni Jafo (hayupo pichani) wakati akizungumza kwenye mafunzo ya uongozi kwa viongozi hao. ******* |
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selmeni Jafo ametoa wito kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa ya Tanzania Bara kusimamia vyema kampeni ya kabambe ya hifadhi na usafi wa mazingira.
Jafo amesema hayo leo Julai mosi, 2021 alipozungumza na viongozi hao wakati wa mafunzo ya uongozi yaliyoandaliwa na Taasisi ya Uongozi ambapo alisisitiza zoezi la upandaji wa miti milioni 1.5 kwa kila Halmashauri ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Makamu wa Rais.
Aliwaomba washiriki kikamilifu katika kusimamia Kampeni hiyo kabambe iliyozinduliwa hivi karibuni na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ili kuhifadhi mazingira na kuweka mikoa katika hali ya safi.
“Ndugu zangu Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala tulikutana na Mawaziri takriban wanane kujadili kuhusu kero ya kelele katika nyumba za burudani, tumeweka maazimio na miongozo ambayo muda si mrefu mtaipata. NEMC (Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira) ni wasimamizi katika eneo hilo lakini maafisa mazingira wa mikoa na wilaya watakuwa na jukumu la kusimamia kule chini niwaombe sana twendeni tukalisimamie hili,” alisema Jafo.
Aidha, Waziri huyo aliwasihi kutumia Kamati za Amani za mikoa yao ziweze kukaa kwa pamoja kuangalia namna bora yua kulisimmaiai suala la kelele katika nyumba za ibada.
Pia alisisitiza usimamizi wa katazo la mifuko ya plastiki ambalo linaendelea kutekeleza katika mikoa yote ya Tanzania Bara kuhakikisha nchi inakuwa salama na safi.
0 comments:
Post a Comment