Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Bw. Joseph Butiku akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (wa kwanza kulia), Mtandao wa Uongozi wa Wanawake Afrika (AWLN) pamoja na baadhi pamoja na baadhi ya viongozi wa Shirika la Kimataifa la kutetea Haki na Maendeleo ya Wanawake (UN Women) leo jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiongea na baadhi ya viongozi na maafisa wa Mtandao wa Uongozi wa Wanawake Afrika (AWLN) pamoja na Taasisi ya Mwalimu Nyerere (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na viongozi na maafisa wa Mtandao wa Uongozi wa Wanawake Afrika (AWLN) wafanyakazi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere pamoja na Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiongea na baadhi ya viongozi na maafisa wa Mtandao wa Uongozi wa Wanawake Afrika (AWLN) pamoja na Taasisi ya Mwalimu Nyerere leo jijini Dar es Salaam
************
Mtandao wa Uongozi wa Wanawake
Afrika (AWLN) kwa kushirikiana na Taasisi ya Mwalimu Nyerere umepewa changamoto
ya kukuza na kusimamia masuala ya umoja na amani katika Bara la Afrika ili
kuleta maendeleo ya watu.
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ametoa wito huo wakati
alipokutana na Mtandao huo pamoja na Taasisi ya Mwalimu Nyerere ikishirikiana
na Shirika la Kimataifa la kutetea Haki na Maendeleo ya Wanawake (UN Women) leo
jijini Dar es Salaam
“Agenda yetu ni muhimu,
hamuwezi kusema kuwa tuna maendeleo kama hakuna amani…….amani ni sehemu ya
Diplomasia ya Uchumi, kama amani huwezi kuitafuta kwa njia nyingine tuseme
amani ni maendeleo na maendeleo ni amani,” Amesema Balozi Mulamula
Balozi Mulamula ameongeza
kuwa, kwa kuzingatia kwamba amani ni matokeo ya haki juhudi zinahitajika katika
kuhamasisha na kuunga mkono ushiriki kamili wa wanawake kama wadau muhimu wa
kulinda na kutetea amani.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji
wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Bw. Joseph Butiku amesema kuwa Taasisi yake ina
jukumu la kuhakikisha kuwa amani na haki zinapatikana hasa katika ukanda wa
Maziwa Makuu.
“Tumepokea changamoto
tuliyopewa na Mhe. Waziri na mimi ninakubaliana na yeye kabisa kuwa
tushirikiane na wanawake katika kuhamasisha na kutunza amani na haki hasa kwa
kushirikiana na wanawake ambao wamekuwa na mchango mkubwa sana wa kutunza amani
na kuwa hakuna mpaka na yote yanawezekana,” Amesema Bw. Butiku.
Mtandao wa Uongozi wa Wanawake
Afrika (AWLN) na UN Women umekuwa ukishirikiana katika kuisaidia Tanzania
kuandaa Mpango kazi wa Kitaifa wa Utekelezaji wa ajenda ya wanawake, amani na
usalama ya Maamuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Na. 1325.
0 comments:
Post a Comment