KATIBU Mkuu idara kuu ya maendeleo ya jamii,Dokta John Jingu amevitaka vyuo vya maendeleo ya jamii nchini kutoa elimu ambayo itakuwa ni nyenzo na silaha ya kupambana na changamoto zilizopo katika jamii na kuweza kuleta matokeo chanja.
Dakta Jingu aliyasema wakati alipotembelea chuo Cha maendeleo ya jamii Monduli Mkoani Arusha ambapo pia ametembelea na kujionea miradi mbalimbali ya wananchi iliyofanikishwa na chuo hicho kwa kushirikiana na wananchi kupia kitengo cha ujasiamali cha chuoni hapo. .
Alisema kuwa,kama wizara imekuwa ikisisitiza vyuo hivyo kuhakikisha wanatoa elimu ambayo itakuwa ni silaha ya utatuzi wa changamoto mbalimbali katika jamii ili uwepo wa vyuo hivyo uweze kutambulika kwa vitendo zaidi.
"unajua unaposema upo chuo unasomea kozi fulani mjue kabisa elimu sio sifa tu ama cheti bali jamii yenyewe inatakiwa ikutambua kwa kazi zako unazozifanya kwani ndizo zitaweza kukutambulisha kwa jamii katika kuhakikisha elimu uliyoipata italeta majibu kwenye matatizo yaliyopo."alisema
Hata hivyo katibu mkuu huyo alifurahishwa na miradi mbalimbali ya kijamii iliyoanzishwa na chuo hicho ambayo bado wananchi wanaendelea kuitekeleza ambayo imewasaidia Sana kujikwamua kiuchumi hivyo kukimwagia sifa chuo hicho kwa ubunifu mkubwa wa kuleta mabadiliko katika jamii.
Naye kaimu Mkuu wa chuo cha maendeleo ya jamii Monduli ,Elibariki Ulomi alisema kuwa,wamekuwa wakitekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika jamii inayowazunguka ikiwemo ufugaji wa kuku,ng'ombe,ambayo imewasaidia kwa kiasi kikubwa Sana kujikwamua kiuchumi.
Alisema kuwa,chuo hicho kimekuwa kikitekeleza kwa vitendo elimu wanayoitoa chuoni hapo ambapo wameweza kuibadili jamii hiyo ya wafugaji kwa kusaidia miradi mbalimbali ya ujasiriamali sambamba na kutoa elimu namna ya kuhifadhi fedha zao wenyewe na kuweza kukopeshana.
Wakizungumzia namna walivyonufaika na chuo hicho wanakikundi cha Tuinuane kilichopo Monduli juu ,walisema kuwa,chuo hicho kimeweza kuwapatia mafunzo mbalimbali namna ya ufugaji bora wa kisasa wa ng'ombe na kuku ambapo wameweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na mradi huo na kuondokana kuwa tegemezi.
Katibu wa kikundi hicho ,Anna Losiloyi alisema kuwa,kikundi hicho kina jumla ya wanachama 30 ambapo wameweza kuwa na kuku Mia moja na ng'ombe mmoja huku wakijishughulisha na biashara ya kushona shanga pamoja na bangili ambazo wamekuwa wakiwauzia watalii na kuweza kutunisha kikundi chao.
Aidha kikundi hicho kimefika mbali zaidi kwa kumwomba Katibu Mkuu kuwazindulia rasmi kikoba ambacho kitawasaidia kuweka fedha zao ili waweze kukopeshana .
0 comments:
Post a Comment