Nafasi Ya Matangazo

August 26, 2019

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa. Joyce Ndalichako akimpongeza Makamu Mkuu wa Taasisi ya Nelson Mandela Prof. Emmanuel Luoga baada ya kuzindua Kituo cha Umahiri cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa. Joyce Ndalichako akikata utepe kuashiria uzinduzi wa wa Kituo cha Umahiri cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano uliofanyika katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa. Joyce Ndalichako akizungumza na wajumbe (Hawapo pichani) walioshiriki katika uzinduzi wa Kituo cha Umahiri cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano uliofanyika katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Umahiri cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano uliofanyika katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa. Joyce Ndalichako pamoja na wajumbe walioshiriki katika uzinduzi wa Kituo cha Umahiri cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wakifatilia mada zilizokuwa zikiwakilishwa katika uzinduzi huo katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa. Joyce Ndalichako akijadili jambo na Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Nelson Mandela Profesa Lughano Kusiluka wakati wa Uzinduzi wa Kituo cha Umahiri cha TEHAMA.
***************
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa. Joyce Ndalichako amezindua Kituo cha umahiri cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Afrika Mashariki @ Centre of Excelence for ICT in East Afrika kilichoanzishwa katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST )Arusha, Tanzania.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Profesa. Ndalichako amesema kituo hicho kilichofadhiliwa na Serikali ya Ujerumani kinalenga kuwajengea uwezo watanzania pamoja na wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika kuleta maendeleo kwa ikiwa ni pamoja na kutoa ufadhili wa masomo ya shahada za uzamili “Masters”.

Waziri Ndalichako amesema Mwongozo wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu unatambua nafasi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kama nyenzo muhimu katika kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nyanja mbalimbali yakiwemo masuala ya viwanda, uchumi na maeneo mengine akitolea mfano mifumo ya fedha inayotumia TEHAMA inavyotumika afrika mashariki.

“Teknolojia na ubunifu kwa ujumla ni nyenzo muhimu katika kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na tunapozungumzia uchumi wa viwanda hatuwezi kufanikiwa kama hatutatoa kipaumbele katika teknolojia, lakini pia kama hatuta kuwa makini katika kutumia tafiti na uvumbuzi katika juhudi mbalimbali za maendeleo” amesisitiza Prof. Ndalichako

Waziri Ndalichako amewashukuru wafadhili wa kituo hicho serikali ya Ujemani ambao tayari wametoa kiasi cha Euro Milioni 1.384 ambayo ni takriban Shilingi Bilioni 3.5 za Kitanzania kati ya Euro Milioni 4 thamani ya mradi mzima utakaotekelezwa kwa miaka minne hadi 2021. Aidha amewashukuru washirika wote wa kituo hicho na kuwataka wanafunzi waliochaguliwa kuanza masomo katika kituo cha CENIT@ EA kutumia fursa hiyo vizuri kwa kusoma kwa bidii na kuonyesha vipaji vyao ili waweze kupata ujuzi katika fani ambaowataitumia katika kuleta maendeleo katika nchi wanazotoka.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza katika uzinduzi huo, ameishukuru Taasisi ya NM- AIST kwa kuendelea kushirikiana na Wilaya ya Arumeru katika kutekeleza miradi ya maendeleo na kwa kuanzisha Kituo cha Umahiri cha TEHAMA. Wakati huohuo ameishauri taasisi ya Nelson Mandela kuhakikisha kituo hicho hakiwi cha wanawataalama pekee bali pia huduma zake zisaidie wananchi hasa wakulima katika kuongeza tija katika kilimo na mazao na kusaidia kutoa mbinu bora za kilimo kupitia tafiti zitakazokuwa zikifanyika.

Naye Kaimu Mwenyekiti wa Baraza wa taasisi hiyo, Profesa Lughano Kusiluka amesema kituo hicho ni cha Jumuiya ya Afrika Mashariki ambacho kitakuwa kikifundisha wanafunzi katika ngazi za shahada ya umahiri katika teknolojia ya mambo simu , hasa masuala ya usalama wa matumizi ya simu na mawasiliano. Amesema kwa sasa kimeanza na wanafunzi 27 kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Masahariki ambapo Tanzania imetoa wanafunzi 10 kati ya hao.

Naye Meneja Mradi wa Kituo cha Umahiri cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka giZ Simon Hochstein, amesema serikali ya ujerumani itaendelea kufadhili miradi mbalimbali katika Elimu ya Juu na kuwata wataalamu kuandaa maandiko ya miradi ili kupata fedha kama ilivyokuwa katika mradi wa Kituo hicho cha Umahiri.
Posted by MROKI On Monday, August 26, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo