Nafasi Ya Matangazo

February 15, 2019

SHIRIKA la ndege linaloongoza Tanzania, Precision Air limetangaza kuanza rasmi kwa safari zake kati ya Dar es Saalaam – Dodoma na Kiilimaanjaaro-Dodomma kuanzia tarehe 1, Aprili 2019. 

Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na shirika hilo hapo jana Meneja Masoko na Mahusiano Bw.Hillary Mremi, amesema kwamba Precision Air itakua ikafanya safari sita kwa wiki kuelekea Dodoma, kila siku ya Jumatatu,Jumanne,Jumatano, Alhamisi,Ijumaa na Jumamosi. Taarifa hiyo inaeleza zaidi kua Jumatano na Ijumaa safari za Dodoma zitakua zikipitia Kilimanjaro na kwa siku zilizobakia safari ziatakua ni za moja kwa moja. 

“Safari zetu hizi mpya zitaiiunganisha Dodoma na mikoa mingine kama Mtwara, Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Nairobi kupitia Dar es Salaam na Kilimanjaro. Abiria kutoka maeneo haya wataweza kuunganisha safari zao kuelekea Dodoma kupitia mtandao wetu wa safari, na hivyo kuunganisha jamii jambo ambalo ni moja kati ya malengo yetu makuu.” Aliongeza Bw.Mremi. 

Taarifa hiyo inaeleza zaidi kua kwa safari za moja kwa moja Ndege itakua ikiondoka Dar es Salaam saa 3:15 Asubuhi na kufika Dodoma saa 4:20 Asubuhi, huku kwa safari za kupitia Kilimanjaro Ndege itakua ikondoka Dar es Salaam saa 8:00 Mchana na kufika Dodoma saa 10:15 Mchana. 

Kwa safari za moja kwa moja kutokea Dodoma, Ndege itakua ikiondoka saa 4:45 Asubuhi na kufika Dar es Salaam saa 5:50 Asubuhi, huku kwa safari za kuptia Kilimanjaro Ndege itakua ikiondoka saa 11:15 Jioni na kuwasili Kilimanjaro saa 12:15 Jioni na Dar es Salaam saa 2:05 usiku. 

Shirika la Ndege la Precision Air lilianzishwa mwaka 1993 kama shirika binafsi la ndege za kukodi, likifanya safari zake kusafirisha watalii katika vivutio vya utalii kama Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Bonde la Ngorongoro pamoja na Visiwa vya Zanzibar. 

Sasa Shirika hilo lenye makoa yake makuu katika Jiji la Dar es Salaam limeendelea kukua na kuwa moja ya mashirika yanayo heshimika katika ukanda wa Africa Mashariki na Africa kwa ujumla.Ikifanya safari zake kutokea Dar es Salaam, Precision Air inasafiri kuelekea Arusha, Bukoba, Kilimanjaro, Mtwara, Mwanza, Tabora, Kahama, Zanzibar,Nairobi na Entebbe. 
Posted by MROKI On Friday, February 15, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo