Nafasi Ya Matangazo

December 19, 2018


 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Richard Mayongela akimweleza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (kulia), changamoto zinazoikabili Mamlaka hiyo, wakati alipotembelea kukagua miundombinu mbalimbali kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza na Menejimenti na Waandishi wa Habari baada ya kufanya ziara ya kukagua miundombinu ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela.


Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (kulia) jana akizungumza na Wafanyakazi wa Kampuni ya inayotoa huduma kwa abiria na mizigo ya Swissport Tanzania, Bi. Sarah Mlawa (kushoto) na Fliora Temba, alipokuwa akikagua miundombinu ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).


 Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (kulia) akimsikiliza Msimamizi Kitengo cha Mitambo, Bw. Gregory Kosamu (wa pili kushoto) aliyekuwa akielezea mifumo ya Kiyoyozi ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA). Watatu kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw.

Roichard Mayongela na kushoto ni Kaimu Meneja Matengenezo na Huduma za
Kiufundi, Bi. Diana Munubi.

 Madereva wanaotoa huduma ya usafiri wa taxi katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), wakizungumza na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe alipokuwa akikagua miundombinu ya Kiwanja hicho jana.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard Mayongela, ameahidi kufanya Maboresho makubwa katika Miundombinu ya Viwanja vya Ndege Tanzania na katika kuhamasisha kasi ya utendaji ya wafanyakazi katika Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania.

Hayo ameyazungumza mbele ya Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe katika mkutano na waandishi wa habari baada ya kufanya ukaguzi wa miundombinu katika jengo la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).  

Awali Waziri Kamwelwe alianzia ziara yake Katika Kiwanja cha Ndege cha Songwe na kubaini kwamba njia ya kuruka na kutua ndege imejegwa chini ya kiwango na mkandarasi lakini pia alipotua JNIA alibaini pia baadhi ya changamoto.

Kufuatia hatua hiyo Waziri Kamwelwe ametoa maagizo kwa TAA kwamba kuanzia Januari mwakani kuwe na mabadiliko katika namna ya utendaji.

“Nawaomba ndugu zangu kuanzia Januari mwakani mbadilike na kama mtu hata badilika basi tutamtoa. Malalamiko ya watu mimi nayapokea na ninayafanyia kazi, kwa maana hiyo ni vyema pia muyafanyie kazi”, alisema Mhandisi Kamwelwe.

Mayongela akizungumza kwa niaba ya Menejimenti katika kikao hicho amebainisha kwamba ujio wa Waziri ni changamoto kwa watendaji wote wa TAA kila mtu ajithimini katika kipindi hiki na kukaa tayari kwa ajili ya maboresho makubwa na utendaji wa kasi wa Mamlaka.

“Kwa niamba ya Wenzangu tunakuahidi kwamba kuanzia januari mwaka unapoanza tutajitahidi kufanya kazi kwa weledi na kwa uadilifu Mkubwa. Kwa upande wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere kuendelea kulalamikiwa kwa kwa mambo madogo madogo ya kiutendaji haioendezi na ni aibu kwetu, mimi mwenyewe kama mtendaji mkuu nitachukua hatua na kuhakikisha kwamba tunakipa hiki kiwanja
kipaumbele”.

Hatahivyo, Waziri Kamwelwe amewatakia watanzania wote heri ya sikukuu za mwisho wa Mwaka na kuwaasa kwamba watumie hii nafasi kujiandaa ili kuja kufanya kazi vizuri mwakani.
Posted by MROKI On Wednesday, December 19, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo