Nafasi Ya Matangazo

December 18, 2018


Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kuutarifa umma kuwa kesho tarehe 19/12/2018, itafunga kwa muda barabara ya Morogoro sehemu ya Kimara Stop Over hadi Temboni Wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 6.00 mchana.

Taarifa iliyotolewa kwa umma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Joseph Nyamhanga inasema Kufungwa kwa muda barabara hii kunatokana na kuwepo kwa sherehe ya uwekaji wa jiwe la msingi la upanuzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 19.2 kutoka Kimara hadi Kibaha kuwa njia nane (8) itakayofanyika eneo la Kimara Stop Over.

“Wizara inashauri watumiaji wa barabara hiyo kutumia barabara mbadala kwa muda wote ambao barabara hiyo itakuwa imefungwa kwa muda” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha, Wizara inawaomba radhi watumiaji wote wa barabara hiyo kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Posted by MROKI On Tuesday, December 18, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo