
Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na baadhi ya washiriki wa maonesho wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani Aprili 28, 2018 iliyoadhimishwa Kitaifa Mkoani Iringa.

Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwasili katika Viwanja vya Kichangani Mkoani Iringa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani Aprili 28, 2018.

Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akitia saini katika kitabu cha wageni alipotembelea banda la maonesho la OSHA wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani Aprili 28, 2018 Iringa.

Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiangalia mfano wa namna bora ya kumuokoa mfanyakazi pindi apatapo ajari sehemu ya kazi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani Aprili 28, 2018 Iringa.

Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Mzee Juma Nyinge aliyetembelea katika mabanda ya maonesho wakati wa Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani Aprili 28, 2018. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

Afisa Mahusiano na jamii kutoka Kampuni ya Acacia Bi. Agripina Joseph akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea banda lao wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani.

Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiuliza swali kwa Afisa Usalama kazini Bw. Mlewa Mustapha kutoka Mgodi wa Buzwagi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani.

Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akipokea zawadi kutoka kwa Kampuni ya Acacia waliposhiriki katika maonesho ya kuadhimisha Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani mkoani Iringa.
Mwalimu
wa wasioona Steven Changalo akiandika jina la mhe.Waziri Mhagama kwa
kutumia vifaa wezeshi alipotembelea banda la Chama cha Walimu Tanzania
(CWT) katika maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi
Duniani mkoani Iringa.
Waziri
wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mhagama akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw.Erick
Shitindi anayeshungulikia Kazi,Ajira, Vijana na wenye ulemavu.
Kaimu
Mtendaji Mkuu OSHA Bi.Khadija Mwenda akizungumza jambo wakati wa Kilele
cha Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani yaliyoadhimishwa
mkoani Iringa.
Katibu
Mkuu wa Ofisi hiyo Bw.Erick Shitindi anayeshungulikia Kazi,Ajira,
Vijana na wenye ulemavu akitoa salamu kwa washiriki wa Maadhimisho ya
Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani yaliyofanyika mkoani
Iringa.
Waziri
wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mhagama akitoa vyeti kwa washindi wa maonesho ya Siku ya Afya na
Usalama Mahali Pa Kazi Duniani yaliyofanyika mkoani Iringa.
Waziri
wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mhagama akihutubia wananchi na washiriki waliohudhuria wakati
Maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani
yaliyofanyika mkoani Iringa.
Waziri wa Nchi Ofisi
(Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
(katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa OSHA
pamoja na watendaji wa Idara ya Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu
wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani
yaliyofanyika mkoani Iringa.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
***********************
Serikali imedhamiria
kuendelea kukomesha ajira hatarishi za watoto ili kuhakikisha kuwa watoto
wanalindwa na kuwapa nafasi stahiki kulingana na sheria na kanuni zilizopo
nchini.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na
Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipohudhuria katika kilele cha Siku
ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 28 Aprili ambapo Kitaifa ilifanyika
Mkoani Iringa.
Waziri alieleza kuwa,
katika mapambano haya ya ajira hatarishi kwa watoto ni moja ya utekelezaji wa
kampeni zinazolenga kuharakisha utekeleezaji wa vipaumbele vilivyomo kwenye
lengo namba (8) la Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ambalo ni kuboresha
mazingira ya wafanyakazi na kukomesha ajira mbaya kwa watoto.
“Tuendelee kupiga
vita ajira mbaya kwa watoto kwa kuzingatia kampeni zilizopo hasa ile ya
kuboresha mazingira ya wafanyakazi ifikapo mwaka 2030 pamoja na kukomesha ajira
mbaya za watoto ifikapo mwaka 2025,” alisema Waziri
Waziri aliongezea
kuwa katika kuhakikisha watoto wanakuwa na mazingira salama , Lazima kuwe na
mikakati ya pamoja baina ya utatu katika
masuala ya kazi na ajira ikiwemo na kujenga utamaduni wa kujikinga na vihatarishi
sehemu za kazi vinavyoweza kusababisha kuhatarisha afya na usalama wa
wafanyakazi.
Aidha kama Taifa
lazima tuoneshe umuhimu wa kuhakikisha kampeni hii inakuwa na matokeo chanya na
kuendelea kuwa na Taifa lenye maendeleo.
Waziri aliongezea
kuwa kulingana na Matokeo ya Utafiti wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali uliofanyika mwaka
2014 na matokeo yake kuchapishwa mwaka 2016 ulibainisha kuwa, hali ya ajira hatarishi za watoto kuzidi kuwa mbaya zaidi
katika sehemu za mashambani, sekta ya madini, misitu na uvuvi.
“Kwa mujibu wa taarifa
za Mtakwimu Mkuu wa Serikali za mwaka 2014 zilibaini kuwa watoto wenye umri
kati ya miaka 5-17 walioko kwenye ajira ni takribani
milioni 4.2 ambayo ni asilimia 28.8 ya wafanyakazi wote na kati ya hao asilimia
21.5 wako kwenye ajira hatarishi hususan sehemu za mashambani ambako asilimia
35.6 ya wafanyakazi wote ni watoto”,alisisitiza Mhe.Waziri
Kwa upande wake Kaimu
Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda alieleza kuwa wataendelea kutekeleza
majukumu yao kwa kuhakikisha sheria zilizopo zinafuatwa bila kukiukwa hususan
kwa makundi maalum iliwemo yale ya vijana na makundi ya watu wenye ulemavu.
“kwa kuwa Vijana
wadogo ndiyo nguvu kazi ya taifa hivyo wanastahiri kulindwa na kuangaliwa kwa
jicho la pekee ili kuwa na kizazi endelevu,”alisema Mwenda
AWALI
Aprili 28 ya kila
mwaka ni siku ya Kimataifa ya kuadhimisha masuala ya Afya na Usalama Mahali Pa
Kazi, ambapo huwa na Kauli Mbiu inayotumika duniani kote ambayo inatolewa na
Shirika la Kazi la Duniani.Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kizazi Salama chenye
Afya – Generation Safe and Health”.Kaulimbiu
hiyo ili kuendana na mazingira ya nchi yetu iliboreshwa na kuwa “Kizazi Salama Chenye Afya kwa Uchumi wa
Viwanda –Generation Safe and Health
for Industrial Economy”.




0 comments:
Post a Comment