Nafasi Ya Matangazo

October 17, 2017

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiongea na viongozi wa serikali ya kata ya Pandagichiza wakiwemo watendaji,Sungusungu,wakulima na Wafugaji, akiwasisitiza kushiriki na kuhamasisha wananchi kuitikia zoezi la upigaji chapa mifugo kwa kuwekwa alama ya serikali
Baadhi ya viongozi wa Serikali ya Kata ya Pandagichiza ,wakiwamo Sungusungu, wakulima na wafugaji wakimsikiliza mkuu wa wilaya kwenye uzinduzi wa upigaji chapa mifugo .
Ofisa mifugi wilaya ya Shinyanga William Kidua akipiga chapa mifugo ya Kijiji cha Shilabela Kata ya Pandagichiza baada ya zoezi la upigaji chapakuzinduliwa  na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Mkuu wa idara ya mifugo na uvuvi kutoka Halmashauri ya Shinyanga Omari Kamata ,akielezea faida za upigaji chapa mifugo.
Daktari wa mifugo kutoka halmashauri ya Shinyanga Vijijini Clement Baksilo ,akielezea faida za upigaji chapa mifugo kuwa endapo mfugo ukiwa hata mnadani ubainika kuwa na ugonjwa itasaidia kubainika unatoka wapi na itakuwa rahisi kuwahi kwenda kutoa tiba mahali hapo na kuokoa mifugo mingine isipate magonjwa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amewataka wafugaji kutii maagizo ya serikali ya kupeleka mifugo yao kuwekewa chapa ya Serikali ili itambulike kisheria na kuwa kinga ya migogoro ya wafugaji.
Akizungumza jana Jumatatu Oktoba 16,2017 kwenye uzinduzi wa upigaji chapa mifugo wakati akiongea na viongozi wa serikali ya kata ya Pandagichiza,Matiro alisema upigaji chapa mifugo hiyo una faida kubwa kwa wafugaji ikiwemo kuzuia migogoro ya wafugaji.
Alisema upigaji chapa mifupo ni agizo la serikali kutoka kwa waziri mkuu Kassim Majaliwa na mfugaji ambaye atakaidi agizo hilo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
"Nampongeza waziri mkuu kwa agizo la upigaji chapa mifugo na tangu zoezi hili lianze kufanyika hakuna mgogoro wowote wa wafugaji uliotokea",alisema Matiro.
Aidha aliwataka wafugaji kujenga utamaduni wa kufuga kisasa kwa kuvuna mifugo yao na kuwekeza pamoja na kujenga makazi yao kuwa mazuri na siyo kuwa na idadi nyingi ya mifugo halafu waanishi maisha mabaya bila hata ya kuwa na kitanda.
Naye mkuu wa idara ya mifugo na uvuvi kutoka halmashauri ya Shinyanga Vijijini Omari Kamata ,alizitaja Sheria ambazo zitachukuliwa kwa mfugaji atakaye kaidi agizo hilo la upigaji chapa mifugo ,kuwa ni faini ya shilingi 300,000/= hadi 600,000/= au kifungo cha Miezi Sita hadi Mwaka mmoja.
Alisema katika halmashauri hiyo kuna jumla ya ng'ombe 344,736 na waliopigwa chapa ni ng'ombe 79,164 tangu zoezi hilo lilipoanza June 20 mwaka huu.
Aidha aliongeza kuwa katika kata hizo mbili za Mwalukwa na Pandagichiza ambalo zoezi hilo la upigaji chapa limezinduliwa leo na mkuu huyo wa wilaya katika kijiji cha Shilabela ambapo  ng'ombe 17,117  wanaoanzia umri wa miezi sita wanatarajiwa kupigwa chapa.
Nao baadhi ya wafugaji walisema awali waligomea zoezi hilo kutokana na taarifa za awali kutolewa ndivyo sivyo ,lakini kutokana na maelezo yaliyotolewa na mkuu huyo wa wilaya wameahidi kutii maagizo hayo na kupeleka mifugo yao kupigwa chapa.
Posted by MROKI On Tuesday, October 17, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo