Katibu Mkuu wa Umoja wa
Wanawake Tanzania (UWT), Amina Makillagi, amewataka wagombea na wajumbe wote wa
mikutano mikuu ya wilaya kwenye Uchaguzi wa jumuiya hiyo ngazi ya wilaya
utakaofanyika leo, tarehe 21/9/2017 kuzingatia maadili ya Chama na UWT.
"Kubwa ni kutotoa wala kupokea rushwa. UWT imejiandaa vizuri kuhakikisha inafuatilia nyendo zozote ovu zitakazojitokeza katika Uchaguzi. Mgombea yeyote atakayetoa rushwa atachukuliwa hatua za kinidhamu kabla na baada ya Uchaguzi kuisha ikiwa ni pamoja na kuvuliwa nafasi ya uongozi iliyopatikana kwa mazingira tatanishi", amesema Makilagi.
Makillagi ambaye amewatakia uchaguzi mwema wanachama wote wa UWT, amesisitiza kuwa rushwa haitavumilika na kwa mjumbe yeyote atakayepokea rushwa na kwamba kanuni zilizopo zitamuwajibisha ipasavyo.
0 comments:
Post a Comment