Pamoja kwa ajili ya Amani: Heshima, Usalama na Utu kwa Wote
Hii Siku ya Kimataifa ya Amani huadhimisha nguvu ya ushirikiano wa kimataifa katika kujenga ulimwengu wa amani na endelevu.
Jambo hili linazidi kuwa ni la muhimu sana hasa wakati huu tunapokumbana na changamoto zisizo za kawaida.
Nguvu
mpya za mgawanyiko zimeibuka, zikieneza chuki na kuondoa kuvumiliana.
Ugaidi unachochea vurugu, wakati misimamo mikali inapandikiza sumu ndani
ya fikra dhaifu za vijana.
Katika
maeneo maskini zaidi ya dunia na yasiyo na maendeleo, majanga ya asili
yanayohusiana na hali ya hewa yanazidisha hali ya kukosa utulivu,
yakiongeza idadi ya watu wanaolazimika kuhama makazi yao na kuongeza
zaidi hatari ya kutokea kwa vurugu.
Vikwazo
vya kuifikia amani vina utata mwingi na ni vigumu sana - hakuna nchi
moja peke yake inayoweza kuviondoa vikwazo hivyo. Jambo hili linahitaji
aina mpya ya mshikamano na hatua za pamoja, na kuanza kuchukua hatua
hizo mapema iwezekanavyo.
Hiki
ndicho kilichoko katika moyo wa wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa, Antonio Guterres, kuongeza jitihada zinazolenga kuendeleza
amani, kuzishirikisha Serikali na mashirika ya kiraia, pamoja na jumuia
za kimataifa na za kikanda.
Mabadiliko yanaenea duniani kote kwa kasi kubwa – ni lazima lengo letu
liwe kuyapokea mabadiliko hao katika misingi ya haki za binadamu, kuyapa
mwelekeo chanya utakaotupeleka kwenye dunia iliyo ya haki zaidi,
jumuishi zaidi na endelevu zaidi.
Utamaduni
wa amani ni utamaduni wa mazungumzo na kuzuia uvunjifu wa amani, na
katika muktadha huu, jukumu la Umoja wa Mataifa halijawahi kuwa la
muhimu sana kama wakati huu. Agenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu
inathibitisha kwamba "hawezi kuwa na maendeleo endelevu bila amani na
hakuna amani bila maendeleo endelevu".
Moyo
huo huo unaungwa mkono na maazimio ya Umoja wa Mataifa kupitia Baraza
la Usalama na Mkutano Mkuu ya mwaka 2016 yanayohusu “amani endelevu”.
Tunahitaji
namna mpya yenye kina zaidi, itakayoshughulikia sababu za msingi, na
kuimarisha utawala wa sheria na kukuza maendeleo endelevu, yote haya
katika misingi ya majadiliano na kuheshimiana.
Hii
ndiyo dira ya hatua zote za UNESCO za kujenga amani kupitia elimu,
uhuru wa kujieleza, majadiliano kati ya tamaduni mbalimbali, heshima kwa
haki za binadamu na kutambua uwepo wa tamaduni mbalimbali na
ushirikiano wa kisayansi.
Katika
hii Siku ya Kimataifa ya Amani, imetupasa wote tuweke upya ahadi na nia
zetu za kujenga umoja wa kimataifa. Ili kuendeleza amani, ni lazima
tuijenge amani kila siku, katika kila jamii, na kila mwanamke na
mwanaume, kwa kufanya kazi pamoja ili kufikia wakati ujao ulio bora
zaidi kwa wote.
0 comments:
Post a Comment