Timu
ya Taifa ya Riadha inayoshiriki mashindano ya Dunia ya riadha
yanayoendelea jijini London inaanza kibarua cha kuipeperusha
bendera yetu leo (Jumamosi 05/08/2017) ambapo mfukuza upepo Failuna
Abdi Matanga atakimbia mbio za mita 10,000 leo .
Failuna atashuhudiwa na maelfu ya watanzania kupitia DStv Muda wa
saa mbili usiku.
Akithibitisha
kuonekana kwa matangazo hayo kupitia DStv, Mkurugenzi Mtendaji wa
Multichoice Tanzania Maharage Chande amesema
DStv imefanya jitihada kubwa na kuhakikisha kuwa watanzania
wanaishuhudia timu yetu ikituwakilisha katika mashindano hayo muhimu
ulimwenguni.
“Tunawahakikishia watanzania burudani hii moja kwa moja kupitia DStv chaneli za Supersport. Tunaamini sote tutakuwa nyuma
yao wachezaji wetu kuwashuhudia jinsi wanavyotuwakilisha” alisema Maharage
“Suala
la watanzania kuwashuhudia vijana wetu wakishiriki katika mashindano
makubwa kama haya lina maana kubwa sana. Vijana
wadogo wakiwaona dada zao na kaka zao wakishiriki mashindano makubwa
kama haya inawatia moyo na kuwapa ari na tamaa ya wao kujitahidi na
kufika hatua kama hizo. Hili ni jambo la muhimu sana na sisi DStv
tunalitilia mkazo sana. Ni njia moja wapo ya kuwashawishi
na kuwatia moyo vijana wetu wanaochipukia na kuwajengea kujiamini”
Baada
ya Failuna anayekimbia mita 10,000, watanzania watashuhudia tena
shughuli pevu siku ya jumapili kupitia DStv kuanzia
majira ya saa nne asubuhi ambapo vidume watatu - Alphonce Felix Simbu,
Ezekiel Jafari Ng’imba na Stefano Huche Gwandu watakuwa wakikata upepo
katika viunga vya jiji la Malkia London ikiwa ni mbio ndefu za kilomita
42.
Baada
ya vidume hao kukamilisha kazi tuliyowatuma, wanawake wetu wa shoka nao
wataingia barabarani ambapo Tanzania inawakilishwa
na Sara Ramadhani Makera na Magdalena Crispin Shauri ambao nao
watafukuza upepo umbali wa kilomita 42 majira ya saa nane mchana.
Patashika yote hii itaonekana DStv.
Wanariadha
wengine wawili wa mbio fupi za mita 5,000 ambao ni Emmanuel Giniki
Gisamoda na Gabriel Gerald Geay watatimka
siku ya Jumatano tarehe 9 Agosti majira ya mbili usiku hii ikiwa ni
raundi ya mchujo na wakifuzu watashiriki fainali ya mita 5,000 siku ya
Jumamosi Agost 12, majira ya mbili usiku. Nao pia watashuhudiwa
mbashara kupitia DStv
Mashindano ya Dunia ya Riadha yalianza rasmi 1983 ambapo Tanzania imewahi kupata medali 1 tu ya Fedha kupitia mwanariadha
Christopher Isegwe kwenye mbio za Marathon 2005 Helsinki Finland.
Ni
mashindano ya pili kwa ukubwa baada ya Olimpiki ambapo nchi 204
zinashiriki mashindano hayo mwaka huu. Tangu kuanzishwa
kwa mashindano hayo mwaka huu ndiyo mwaka ambao Tanzania imeleta timu
kubwa ya wanariadha 8, ambao ina mchanganyiko wa wanaume na wanawake na
pia kuna wakimbiaji wa mbio za uwanjani.
Wanariadha wote wanaoshiriki wamefikia viwango vinavyotakiwa na Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF)
0 comments:
Post a Comment