Rais Dkt John Pombe Magufuli akipokea
hati ya utambulisho kutoka kwa Mhe. Laszlo Eduard Mathe Balozi wa Hungary nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi Kenya leo Machi 23, 2017 Ikulu jijini Dar es salaam.
************
Balozi
wa Hungary hapa nchini mwenye makazi yake Nairobi, Kenya,Lazaro Eduard Mathe
amemhakikishia Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa nchi yake ipo tayari
kushirikiana na Tanzania katika kuendeleza sekta ya viwanda na kwamba
wawekezaji kutoka Hungary wameanza kufanya mchakato wa kujenga kiwanda cha
kuunda mabasi ya abiria.
Lazaro
Eduard Mathe amesema hayo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na
Rais Magufuli muda mfupi baada ya kukabidhi hati zake za utambulisho akiwa ni
miongoni mwa Mabalozi sita waliokabidhi hati hizo.
Pamoja
na nia ya kujenga kiwanda cha kuunda mabasi ya abiria, Lazaro Eduard Mathe
amempongeza Rais Magufuli kwa juhudi kubwa anazofanya kujenga uchumi wa
Tanzania na ameahidi kuwa Hungary itakuza na kuimarisha ushirikiano wake na
Tanzania kwa kuleta teknolojia katika sekta mbalimbali ikiwemo viwanda na
kilimo pamoja na kuwahimiza wawekezaji kuja kuwekeza nchini Tanzania.
Rais Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati ya utambulisho kutoka kwa Dmitry Kuptel Balozi wa Mauritius nchini mwenye makazi yake jijini Maputo nchini Msumbiji leo Machi 23, 2017 Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Dkt John Pombe Magufuli
akipokea hati ya utambulisho kutoka kwa Mhe. Sidibe Fatoumata Kama, Balozi wa Guinea nchini mwenye makazi yake jijini Addis Ababa, Ethiopia, leo Machi 23, 2017 Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Dkt John Pombe Magufuli
akipokea hati ya utambulisho kutoka kwa Lebonaamang Thanda
Mokalake, Balozi wa Botswana nchini mwenye makazi yake jijini Lusaka, Zambia, leo Machi 23, 2017 Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Dkt John Pombe Magufuli
akipokea hati ya utambulisho kutoka kwa Mhe. Adam Maiga ZakariaouBalozi wa Niger nchini mwenye makazi yake jijini Addis Ababa, Ethiopia, leo Machi 23, 2017 Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati ya utambulisho kutoka kwa Mhe. Jean Pierre Jhumun, Balozi wa Belarus nchini mwenye makazi yake jijini Addis Ababa Ethiopia leo Machi 23, 2017 Ikulu jijini Dar es salaam.
*************
Aidha,
Rais Magufuli amepokea hati za utambulisho za Balozi wa Belarus hapa nchini
mwenye makazi yake Mjini Addis Ababa - Ethiopia, Dmitry Kuptel ambaye
amemhakikishia kuwa katika kuimarisha uhusiano na ushirikiano, nchi hiyo
imejipanga kuimarisha uwepo wake barani Afrika kwa kuongeza uwekezaji katika
viwanda na biashara.
Mabalozi
wengine waliowasilisha hati zao za utambulisho ni Fatoumata Kaba Sidibe, Balozi
wa Guinea hapa nchini mwenye makazi yake Mjini Addis Ababa - Ethiopia, Balozi
wa Botswana hapa nchini mwenye makazi yake Mjini Lusaka – Zambia , Lebonaamang
Thanda Mokalake, Balozi wa Niger hapa nchini mwenye makazi yake Mjini Addis
Ababa – Ethiopia, Adam Maiga Zakariaou na Balozi wa Mauritius hapa nchini
mwenye makazi yake Mjini Maputo – Msumbiji , Jean Pierre Jhumun.
Rais
Magufuli amewapongeza Mabalozi wote walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa
nchini na amewahakikishia kuwa Tanzania itaendeleza na kuimarisha zaidi
uhusiano na nchi hizo huku akiwasihi Mabalozi hao kutilia mkazo uhusiano na
ushirikiano katika kiuchumi.
“Nimeambiwa
Mauritius inafanya vizuri katika viwanda vya nguo na uzalishaji wa sukari,
nitafurahi sana kuona wawekezaji wa kutoka Mauritius wanakuja kuzalisha sukari
hapa nchini, nakuomba Mhe. Balozi ukampe ujumbe Mhe. Rais kuwa ninawakaribisha
sana wawekezaji wa kutoka Mauritius” amesema Rais
Magufuli.
0 comments:
Post a Comment