Mkuu
wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo(kwanza kulia) akizungumza na wadau wa maendeleo
Bw. Hans Paul(pili kulia) ambaye amehaidi kujenga viwanja vya michezo ndani ya
kata ya Engutoto na Bw. Jagjit Aggarwal
**************
Na Woinde Shizza,Arusha
WANANCHI kutoka kata ya
Engutoto jijini hapa,wanatarajiwa
kutimiza ndoto zao za muda mrefu juu ya ukosefu wa viwanja baada ya
mfadhili kujitokeza kuwajengea.
Mfadhili huyo Hans Paul
kupitia kampini ya Dharam Singh Hanspaul &son ltd alisema hayo mbele ya
mkuu wa mkoa Arusha kuwa katika kutimiza
adhma ya serikali kusaidia maendeleo ya michezo kwa vijana amejitolea kujenga
viwanja viwili vya michezo.
“Viwanja tutakavyojenga ni kwa
mpira wa miguu na mpira wa Netiboli na
vinatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi milioni 30 fedha za kitanzania na
tunatarajia kuanza ujenzi huo ifikapo mwanzoni mwa mwaka 2017,”Alisema Paul.
Alisema kuwa lengo kuu la kujenga viwanja ni katika kuwawezesha vijana wapate muda wa kujihusiha na michezo ili
kuepukana na tabia hatarishi ambazo zingeharibu ndoto za maisha yao.
Baahi ya wakazi wa kata hiyo
wakizungumzia neema watakayoipata kutoka kwa mfadhili huyo walisema “Ni jambo
la kupongeza kwani vijana wengi wamekuwa hawana mahali pa kufanya mazoezi na
kwa hali hii itasidia sasa kuanza kuona vipaji vya michezo katika kata hii.”
Alisema mmoja wa wakazi hao.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa
Arusha Mrisho Gambo alisema juhudi alizozifanya mfadhili huyo katika sekta ya
michezo ni jambo la heri ambalo linatakiwa liwe mfano kwa wadau wengine katika
kusaidia kuinua michezio katika jamii sambamba na kuwa michezo ni moja ya ajira kwa Vijana .
kawaida mkuu wa mkoa wa Arusha
Mrisho Gambo(kwanza kulia) akizungumza na wadau wa maendeleo Bw. Hans Paul(pili
kulia) ambaye amehaidi kujenga viwanja vya michezo ndani ya kata ya Engutoto na
Bw. Jagjit Aggarwal Na Woinde Shizza,Arusha WANANCHI kutoka kata ya Engutoto
jijini hapa,wanatarajiwa kutimiza ndoto zao za muda mrefu juu ya ukosefu wa
viwanja baada ya mfadhili kujitokeza kuwajengea.
Mfadhili huyo Hans Paul kupitia kampini ya
Dharam Singh Hanspaul &son ltd alisema hayo mbele ya mkuu wa mkoa Arusha
kuwa katika kutimiza adhma ya serikali kusaidia maendeleo ya michezo kwa vijana
amejitolea kujenga viwanja viwili vya michezo.
“Viwanja tutakavyojenga ni kwa
mpira wa miguu na mpira wa Netiboli na vinatarajiwa kugharimu kiasi cha
shilingi milioni 30 fedha za kitanzania na tunatarajia kuanza ujenzi huo
ifikapo mwanzoni mwa mwaka 2017,”Alisema Paul.
Alisema kuwa lengo kuu la kujenga
viwanja ni katika kuwawezesha vijana wapate muda wa kujihusiha na michezo ili
kuepukana na tabia hatarishi ambazo zingeharibu ndoto za maisha yao.
Baahi ya wakazi wa kata hiyo
wakizungumzia neema watakayoipata kutoka kwa mfadhili huyo walisema “Ni jambo
la kupongeza kwani vijana wengi wamekuwa hawana mahali pa kufanya mazoezi na
kwa hali hii itasidia sasa kuanza kuona vipaji vya michezo katika kata hii.”
Alisema mmoja wa wakazi hao.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa Arusha Mrisho Gambo alisema juhudi alizozifanya
mfadhili huyo katika sekta ya michezo ni jambo la heri ambalo linatakiwa liwe
mfano kwa wadau wengine katika kusaidia kuinua michezio katika jamii sambamba
na kuwa michezo ni moja ya ajira kwa Vijana .
0 comments:
Post a Comment