Mkuu wa Masoko na Vinywaji
vikali wa SBL , Stanley Samtu (katikati) akiongea na waandishi wa
habari ( hawapo pichani) katika mkutano wa waandishi wa habari ambapo
alitangaza kuanza kwa msimu wa pili wa shindano la kutafuta DJ aliyobobea katika kuchanganya muziki ambalo linalenga kuibua
na kukuza vipaji vilivyomo ndani ya sekta ya muziki Tanzania.Kulia
kwake ni Meneja chapa wa vinwaji vikali Shomari Shija na kushoto ni DJ
PQ ambaye ndiye Jaji Mkuu katika shindano hilo.
Meneja
chapa wa vinwaji vikali Shomari Shija akifafanua jambo wkwa waaandishii
wa habari katika mkutano huo uliofanyika katika ofisi za SBl Temeke
jijini Dar es salaam,katikati ni jaji mkuu wa shindano hilo Dj PQ na
kushoto mwishoni ni Mkuu wa Masoko na Vinywaji vikali wa SBL , Stanley Samtu .
Meneja
Biashara wa SBL Esther Raphael akimkabidhi mmoja wa washindi
waliofanikiwa kuingia msimu wa pili wa shindano la msimu wa pili wa
shindano la kutafuta DJ aliyobobea katika kuchanganya muziki ambalo
linalenga kuibua na kukuza vipaji vilivyomo ndani ya sekta ya muziki Tanzania.
MaDJ
waliofanikiwa kuingia msimu wa pili wa shindano la SBL la kutafuta DJ
mbobezi kuchanganya muziki wakiwa katika mkutano wa waandishi wa habari
uliofanyika katika ofisi za SBL Temeke Jijini Dar es salaam.
******************
Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imetangaza kuanza kwa awamu ya pili ya miezi mitatu ya shindano la kutafuta DJ aliyobobea katika kuchanganya muziki ambalo linalenga kuibua na kukuza vipaji vilivyomo ndani ya sekta ya muziki Tanzania.
Akizungumza wakati wa kutambulisha awamu ya pili ya shindano hilo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Masoko na Vinywaji vikali wa SBL , Stanley Samtu alisema kuwa shindano hilo linadhaminiwa
na kinywaji cha Smirnof Black Ice linamaanisha pia kuwapa wapenzi wa
muziki kote nchini fursa ya kufurahia vibao vipya vya muziki
vitakavyochezeshwa na ma+DJ walio na vipaji katika sekta hiyo.
“Leo tunatangaza ma+DJ 18 kati ya 40 kutoka mikoa mine ambao wamefanikiwa kuingia katika awamu ya pili ambapo Dar es Salaam wapo 10, Dodoma wawili, Arusha wawili, Morogoro wawili na Mwanza wawili,” alisema.
Kwa mujibu wa Samtu ni kwamba Smirnof Black Ice ni chapa ya kinywaji inayoongoza katika kipengele cha kinywaji maarufu miongoni mwa watumiaji wa tabaka la kati, katika maeneo yaote ya mijini na vijijini.
Tunaamini kwamba kupitia shindano kupitia shindano hili SBL itatoa vipindi vya kufurahisha miongoni mwa wapenzi wa muziki watakaotembelea yatakakofanyika mashindano na wakati huo huo kuwapatia fursa ya kipekee ya kuibua, kukuza na kuangalia vipaji vilivyopo katika ulimwengu wa muziki na ma-DJ.”
Alisema kwamba kundi la vipaji vinavyosakwa katika mashindano hayo ni la vijana walio na umri kati ya miaka 18 hadi 30, ambao kwa mujibu wa Samtu ni kwamba shindano hilo linawafaa wanafunzi walio katika ngazi ya eilimu ya juu pamoja na wanataaluma ambao ni vijana. vijina.
“Zitatolewa zawadi nzuri kwa ma-DJ watakaoshinda,” alisema na kudokeza kuwa zawadi hizo ni pamoja na seti ya vifaa vya kuchanganya muziki, kompyuta mpakato, na mashine ya kuchanganya muziki kwa washindi watatu watakafika fainali.
“Tunatoa wito kwa kwa ma-DJ wote , wasimamizi wa mabaa na wapenzi wa muziki katika miji hii kushiriki kwa wingi katika shindano hili la kuvutia ili waweze kuifurahia sekta ya muziki ya Tanzania,” alisema Samtu.
0 comments:
Post a Comment