Nafasi Ya Matangazo

August 01, 2016

Mmoja wa viongozi wa Kampuni ya vifaa vya umeme wa jua ya Zola, akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kampuni hiyo, jijini Arusha. 
Shughuli za uzinduzi wa duka hilo, jipya la vifaa vya umeme wa jua la Kampuni ya Zola, zikiendelea jijini Arusha. 
Wafanyakazi wa Kampuni ya vifaa vya umeme wa jua ya Zola wakishangilia mara baada ya kukatwa utepe wa kulizindua rasmi duka hilo, jipya jijini Arusha. 
Wananchi wakiwa katika uzinduzi wa duka hilo, jipya la vifaa vya umeme wa jua la Zola jijini Arusha.

Na Mwandishi wetu, 
KAMPUNI ya Off Grid Electric, inayomiliki kampuni ya umeme wa jua ya M-POWER ya Tanzania, imetangaza rasmi leo kubadilisha jina la biashara (brand name) na ufunguzi wa duka lake la mauzo ya bidha zake kwa rejareja hapa nchini.

Ufunguzi huo utawasaidia Watanzania kupata umeme wa jua wenye uhakika kwa bei nafuu kwa matumizi ya majumbani  na katika biashara zao.

Wakati ikiendelea na kujipanua, Off Grid sasa inabadilisha jina la biashara kutoka M-POWER na kwamba kwa sasa itajiuza kwa jina la Zola.

Jina hili la biashara linabeba dhana nzima ya kwamba kampuni hii ina mizizi yake hapa Afrika Mashariki. Neno Zola limetoholewa kutoka katika neno la Kiswahili la Solar (Sola) na hivyo litatumika kama jina la biashara la kampuni ya Off-Grid katika mataifa ya Tanzania na Rwanda wakati kampuni ikijidhatiti kujipanua zaidi barani Afrika.

Hata hivyo, kampuni itaendelea kujulikana kwa jina la Off Grid Electric.

“Kutokana na azma yetu ya kukua zaidi na kufika katika nchi nyingi zaidi hapa barani Afrika, tunahitaji jina la biashara litakalofanya kazi ndani na nje ya jiografia ya Afrika ili kuonyesha mtazamo wetu wa mabadiliko katika utendaji,” alisema mwanzilishi mwenza wa Off-Grid Electric, Bwana Erica Mackey na kuongeza: “Tunaijenga Zola ili iwe kampuni ya umeme wa nguvu ya Sola kwa Afrika nzima”.

Jina ya biashara la Zola litazinduliwa rasmi leo (July 28, 2016) kwa ufunguzi rasmi wa maduka ya mauzo ya bidhaa za Zola Tanzania na Rwanda.

Akizungumza katika uzinduzi huo, mkuu wa ubia wa Zola, Bwana Godfrey Kakembo alisema: “Maduka ya Zola yatawasaidia wateja kujionea jinsi ambavyo bidhaa zetu zinavyfanya kazi na pia kuweza kuagiza ili waweze kufungiwa sola majumbani mwao. Kwa njia hiyo, wateja wataweza kutoa Zawadi ya kudumu kwa ndugu, jamaa na marafiki zao waishio vijijini”.

Katika maduka ya Zola, wateja wataweza kulipa papo hapo na pia wataruhusiwa kuingia makubaliano ya kulipa kidogo kidogo.
Wahudumu kwa wateja watakuwepo muda wote ili kujibu maswali yote yatakayoulizwa na wateja kuhusiana na bidhaa za Zola.

Waanzilishi wa kampuni na wajumbe wa bodi nao pia watakuwepo ili kushuhudia ukataji utepe utakaoashiria ufunguzi rasmi wa duka la Zola jijini Arusha.

Mwezi uliopita, kampuni ya Off Grid Electric ilizindua mpango maalum wa kusaidia kufikisha umeme wa sola unaofaa kwa matumizi ya wajasiliamali wa vijijini. Mpango huo ulizinduliwa huko California katika mkutano wa kilele uliohudhuriwa na Rais wa Marekani Barak Obama.

Mpango huo unajulikana kwa jina la “Kazi na Zola” na unatoa umeme wa kutosha kwa wafanyabiashara chipukizi kutoka Tanzania na Rwanda kuweza kufanya biashara zao bila shida, iwe ni biashara ya kinyozi, kuchaji simu, bar na mgahawa kwa kutumia umeme wa jua.

Kuhusu Off Grid Electric
Off Grid Electric (OGE), Kampuni mama ya Zola ni kampuni kubwa inayotoa huduma ya nishati safi, yenye bei nafuu na inayobadilisha maisha moja kwa moja majumbani. Kampuni inafanya kazi zake Tanzania na Rwanda. Kwa maelezo zaidi, tembelea:  zola.co.tz.
Posted by MROKI On Monday, August 01, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo