Mawakala wa Kanda ya Nyanda juu Kusini waliohudhuria uzinduzi wa
kampeni mkoani wakifuatilia matukio na kutoa mawazo ambapo pia walipata fursa
ya kutoa maoni yao kibiashara
Mawakala wa Kanda ya Nyanda juu Kusini waliohudhuria uzinduzi wa
kampeni mkoani wakifuatilia matukio na kutoa mawazo ambapo pia walipata fursa
ya kutoa maoni yao kibiashara
KAMPENI ya kuwania kujishindia malori ya usambazaji iliyolenga
kuwanufaisha mawakala wa kampuni ya Tanzania Distilleries kupitia
kampeni inayojulikana kama “Nunua,Uza,Shinda na Konyagi inazidi kushika kasi
kadri muda wake wa kumalizika unavyosogea ambapo mawakala wanaendelea kuchuana
kuuza bidhaa za kampuni kwa ajili ya kufikia lengo lililowekwa ili waweze
kushiriki kwenye droo ya kupata washindi itakayofanyika mapema mwezi Oktoba.
Kampeni hiyo ambayo imewalenga wasambazaji katika mikoa yote
nchini itawawezesha washindi 2 kujishindia kila mmoja lori aina ya
Eicher yenye uzito wa tani 3 na pia katika kipindi hiki cha kampeni
wanaendelea kujipatia zawadi mbalimbali.
Akiongelea maendeleo ya kampeni hii baada ya kukamilika zoezi la
uzinduzi wake kwenye kanda za mikoa mbalimbali,Meneja Masoko na Udhamini wa TBL
Group,George Kavishe,alisema kuwa mwitikio wa mawakala katika kushiriki ni
mzuri kinachosubiriwa ni washindi wawili kujinyakulia malori ya
kuwarahisishia zoezi la usambazaji na biashara zao kwa ujumla. SOMA ZAIDI HAPA
“Natoa wito kwa mawakala wetu kuendelea kushiriki katika kampeni hii na
kufikisha malengo ya kuingia kwenye droo kwa kuwa imeandaliwa kwa ajili yao kwa
ajili ya kuwawezesha na tunachosubiri ni kuona magari haya yatachukuliwa na
wasambazaji kutoka kanda gani.
Kavishe alisema lengo kubwa la kampeni hii ambayo imesifiwa na
wasambazaji wa vinywaji vya kampuni hiyo kutokana na kuwa na zawadi kubwa ni
kuwainua kibiashara wasambazaji wa bidhaa za kampuni ikiwemo kuwapatia motisha
kutokana na kushirikiana na kampuni kibiashara.
“TBL Group tunazo Programu mbalimbali za kuwezesha wateja wetu na ndio
maana tumekuwa tukiandaa promosheni mbalimbali zenye lengo la kuwainua kimaisha
ikiwemo kuwapatia mafunzo mbalimbali ya mbinu za kufanya biashara kwa
mafanikio”.Alisema
Alisema kampeni itadumu kwa kipindi cha wiki 12 na wasambazaji
wanaoshiriki wamewekewa viwango vya mauzo; na washiriki wote watakaofikia vigezo
wataingia kwenye droo kubwa ya kupata mshindi mwezi Oktoba mwaka huu .
“Tunaamini kabisa kampeni hii itaongeza ufanisi kwa wasambazaji wetu nao
watoongezea chachu ya manunuzi ya bidhaa zetu”.Alisema.
Baadhi ya mawakala wamepongeza jitihada za kampuni kutenga zawadi kubwa
za promosheni ambazo zitawawezesha washindi kurahisisha biashara zao badala ya
zawadi ndogondogo zisizoweza kumwinua kimaisha mshiriki.
Mmoja wa wauzaji wa bidhaa ya Konyagi kanda ya Kusini aliyejitambulisha
kama Saimon Haule amesema kuwa japo sio mawakala wote watapata malori lakini
watakaobahatika kushinda watakuwa wamepata zawadi ya uhakika na inayofanikisha
biashara kukua. “Kampeni hii ya Konyagi ni kubwa cha muhimu ni kukidhi vigezo
vya kuingia kwenye droo ya kumpata mshindi “.Alisema
0 comments:
Post a Comment