Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad jijini Dar es Salaam mara baada ya kumjulia hali jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye pia
ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad jijini Dar es
Salaam. Maalim Seif amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kumjulia hali na kusema kuwa hali yake ya kiafya inaimarika
siku baada ya siku.
*****************
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtembelea na kumjulia hali
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Maalim Seif Shariff Hamad,
katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam, ambako anapata mapumziko baada ya
kuruhusiwa kutoka hospitali ya Hindu Mandal alikokuwa amelzwa kwa matibabu.
Pamoja na kumpa
mkono wa pole, Rais Magufuli amemuombea Maalim Seif Shariff Hamad kupona haraka
ili aweze kuendelea na shughuli zake kama kawaida.
"Nilishtushwa
sana na taarifa za kuugua kwako, lakini sasa nafurahi kukuona ukiwa mwenye afya
nzuri ikilinganishwa na taarifa nilizozipata hapo awali, nakupa pole sana"
amesema
Rais Magufuli wakati akimjulia hali hotelini hapo.
Kwa upande wake
Maalim Seif Shariff Hamad amemshukuru Rais Magufuli kwa ukarimu na upendo
aliouonesha kwa kumtembelea hotelini hapo, na amewahakikishia watanzania kuwa
hali yake sasa inakwenda vizuri na inazidi kuimarika kila kukicha.
"Sasa hivi
ninaweza kutembea vizuri, kufanya shughuli zote mwenyewe bila ya msaada wa mtu
yeyote yule, na ni matumaini yangu kwamba baada ya muda mfupi, hali yangu
itarudi kama kawaida, nije nishirikiane na watanzania wenzangu katika
kutekeleza majukumu ya nchi yetu" Maalim Seif alimweleza Rais Magufuli.
0 comments:
Post a Comment