MSANII wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wake mpya wa Mama Kijacho
Khalid Ramadhani ‘Tundaman’’ (pichani juu) hatimaye amepata dili la ubalozi wa kampeni ya
kuhamasisha wanawake wa Africa kuhusiana na tamasha la wanawake liitwalo (AFWAB
AMSHA MAMA 2016).
Tamasha hilo ambalo lilianza tangu
mwishoni mwa Desemba mwaka jana, kunako Hoteli ya nyota tano ya The
Tribe na vitongoji vya Nairobi, Kenya, mfanyabiashara mashuhuri na mwenye jina
kubwa music , alifanya bonge la tamasha liliacha gumzo kwa kuvuta maelfu wa
watu kutoka kila kona ya dunia.
Mkurugenzi Mtendaji wa ‘lebal’ ya Candy na Candy Records, Joe Kariuki, (pichani kulia) aliratibu
tamasha maridadi lililojulikana kama Amsha Mama, maalum kwa Wanawake wa
Kiafrika, tamasha lililofanyika katika Hoteli ya kifahari ya Tribe, sehemu
ambayo ni maarufu sana pia kwa wasanii kutoka Marekani, akiwemo Akon.
Tamasha hilo ambalo lengo kubwa lililenga kuzungumzia bayana hali
halisi ya maisha ya mwanamke wa Afrika kuhusu safari yake, mapigano yake
kimaisha, mafanikio, biashara, ubunifu na ushindi wake katika maisha.
Kama mwanaume ambaye siku zote aliye karibu na moyo wa mwanamke ambaye alitaka kumtuza ama kumzawadia kwa
hatua aliyofikia, kumtia moyo, kumhamasisha katika safari yake ya mafaniko
katika jamii hii yenye mfumo dume barani
Afrika. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Akizungumza katika event hiyo,
Joe alisema: "Kuwawezesha wanawake ni muongozo katika jamii, nami nataka kutumia ujuzi wangu
na uzoefu nilionao kujenga jukwaa kwa ajili ya wanawake kukua biashara zao."
Washiriki wengi ambao ambao
wengi wao walisafirishwa kutoka nchi za mbali kwa ajili ya kuhudhuria ‘event’
hiyo, waliunga mkono mawazo ya Joe, mfano Uganda na Italia.
Lisa raia wa Italia alisema: "Dhana ya Amsha Mama ni ya kipekee. Naangalia
wanawake wenye uwezo wa kuzalisha hila zitakazotumika huko Milan. "
Sophie kutoka Uganda, alisema: "Ninawezaje ku-miss hii! Kama mwenyekiti
wa chama chetu cha wanawake 600 nataka kuhakikisha wanapata aina hii ya fursa
kwa ajili ya kuonyesha bidhaa zao na kwa ajili ya kupata mtandao na wanawake
wengine."
Rundo la wanawake waliokuwa na hisia kama hizo, akiwemo mwingine kutoka Copenhagen, Denmark: "Tamasha
haya ndiyo tunahitaji kwa ajili ya kukuza wanawake. Inaonyesha nguvu za
wanawake na mipango yao."
Na katika hilo, Joe anaendeleza jitihada zake za si tu kumwezesha
Mwanamke wa Afrika, bali pia kumuinua, kumtia moyo wake, kumpa mwangaza na kujihusisha
kwake.
Hivyokwa sasa na ndiyo maana ameandaa maonyeshwa makubwa ya wanawake
(AFWAB AMSHA MAMA 2016), yatakayofanyikia katika Uwanja wa Kedong ranch uliopo
katika jiji la Naivasha nchini Kenya Machi 25-27 2016.
0 comments:
Post a Comment