Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame
Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kampuni ya Simu (TTCL), kanda ya
ziwa Peter Kuguru kuhusu nguzo za alama zinazoonyesha sehemu ulikopita mkongo
wa taifa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Mitambo
ya Mawasiliano ya TTCL mjini Shinyanga.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akimuonesha moja ya mifuko inayotumika
kuhifadhi barua Meneja wa Posta mkoa wa
Shinyanga Eugenia Punjira, alipokagua utendaji wa shirika hilo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (katikati) akitoa maelekezo kwa Mkuu wa
Stesheni ya Reli Shinyanga Bw. Baruani Issa (kulia) kuhusu kuanza kutumia jengo
la kuhifadhia mizigo (ICD) katika stesheni hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na sehemu ya wafanyakazi wa Shirika
la Reli Tanzania (TRL) mkoani Shinyanga.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wa sekta za
ujenzi, uchukuzi na mawasiliano kuhusu kufanya kazi kwa umoja na kutekeleza
malengo waliyokubaliana ili kukuza uchumi wa taasisi hizo na kuleta tija.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiwa amesimama juu ya reli ya kati mjini
Shinyanga, mbele ni nyumba ya makazi iliyojengwa juu ya reli hiyo na kuizuia.
****************
Serikali imekemea vikali vitendo
vya baadhi ya wananchi kujenga katika maeneo yenye miundombinu ya barabara na reli
na hivyo kusababisha usumbufu, hujuma na uharibifu wa mali za umma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Prof. Makame Mbarawa ameyasema hayo wakati akikagua sehemu ya njia ya reli ya
kati, mjini Shinyanga na kukuta nyumba iliyojengwa na kuzuia reli. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
“Kazi ya Serikali ni kujenga
Miundombinu na kazi ya wananchi ni kulinda Miundombinu, Mkuu wa mkoa hakikisha
nyumba hii inabomolewa haraka na hatua za kisheria zichukuliwe kwa wote waliohusika
na hujuma hii”, amesema Prof. Mbarawa.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga Bw. Ally Rufunga amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa Serikali
mkoani humo itatekeleza maelekezo yake na kuhakikisha miundominu ya barabara,
reli na mawasiliano inalindwa wakati wote.
Waziri Prof. Mbarawa amewahakikishia
watumishi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), kuwa Serikali iko katika hatua za
kuunganisha TRL na Kampuni Miliki ya Rasilimali za Reli (RAHCO) ili kuongeza
ufanisi wa shirika hilo na kuwataka kuanza kutumia jengo la Hifadhi ya Mizigo
(ICD)iliyojengwa na RAHCO ambalo haijatumika kwa takribani miaka mitatu sasa.
Amekemea vitendo vya uvivu na
hujuma vinavyofanywa na watumishi wasio waaminifu vya kuiba mafuta na kuangusha
mabehewa na hivyo kulisababishia hasara Shirika hilo.
Aidha, Prof. Mbarawa amesema
tayari TRL imeaanza kusafirisha makontena kutoka bandari hadi ubungo ambapo kwa
sasa takribani makontena mia moja yanatoka bandarini na kusafirishwa kwa njia
ya Reli hatua ambayo itahuisha utendaji wa Shirika hilo.
Waziri Prof. Mbarawa amewataka
wafanyakazi wa TRL kutoa ushirikiano kwa Uongozi mpya ili kuwezesha kufikia
malengo yaliyokusudiwa.
“Tutaendelea kusafisha TRL ili
lifanye kazi kwa faida, mchezo wa kuangusha mabehewa na kuiba mafuta ufike mwisho, lazima tuchunguze na sheria ichukue
mkondo wake kwa wote waliofanya vitendo hivyo”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Kwa upande wake, Mkuu wa Stesheni
ya Shinyanga Bw.Baruani Issa ameiomba Serikali kutumia usafiri wa reli kusafirisha
mizigo mingi ili kufufua Shirika hilo na kulinda miundombinu ya barabara.
Waziri Prof. Mbarawa
amewahakikishia watumishi wa TRL kuwa mpango wa kujenga reli ya kisasa Standard
Gauge upo na utatekelezwa kwa awamu ili kuwezesha reli hiyo kubeba mzigo mkubwa
na kuongeza mapato kwa Shirika na kukuza uchumi wa nchi.
Waziri Mbarawa yupo katika
ziara ya kukagua miundombinu ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano katika mikoa ya
kanda ya ziwa ambapo amewataka wasimamizi na wafanyakazi wa TANROADS, TEMESA,
TBA, SUMATRA, TRL,TAA,TMA,TTCL na POSTA kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano
ili kufikia lengo la kuwajengea watanzania miundombinu itakayowafikisha kwenye
uchumi wa kati ifikapo 2025.
0 comments:
Post a Comment