Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na wafanyakazi (hawapo pichani) kuhusu kufanya kazi kwa uadiliafu na uwazi ili kusaidia mashirika hayo kusonga mbele.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa
akifafanua jambo kwa wafanyakazi wa TTCL na POSTA mara baada ya kutembelea na
kuona utendaji kazi wao, jijini Mwanza.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa tatu
kulia) akipata maelezo ya namna mitambo ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL)
inavyofanya kazi kutoka kwa Mtaalamu wa Mitambo (Technician) Edward
Lukungu (wa pili kushoto) wakati wa
ziara ya kutembelea Shirika hilo jijini Mwanza.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa
kwanza kushoto) akipata taarifa ya utendaji wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) kutoka
kwa Meneja Mkoa wa Mwanza Bw. Julius Chifungo (katikati) wakati alipotembelea
ofisi za Shirika hilo jijini Mwanza. Kulia ni Meneja wa TTCL Mkoa wa Mwanza,
Johnbosco Kalista. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa
akiangalia moja ya mitambo ya mkongo wa taifa iliyopo Mkoani Mwanza.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa menejimenti ya TTCL na POSTA alipowatembelea jijini Mwanza.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisalimiana
na watumishi wa TTCL na Posta mkoani Mwanza.
***************
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof.
Makame Mbarawa amewataka watendaji wa Shirika
la Posta Tanzania na Kampuni ya simu ya
(TTCL) kufanya kazi kwa weledi na mtazamo
wa kibiashara ili kuyaongezea
mapato mashirika hayo na hivyo kuendana
na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanaoyotokea
nchini.
Akizungumza na wafanyakazi wa TTCL na POSTA mkoani
Mwanza Prof. Mbarawa amesema kutokana na kukua kwa teknolojia ya mawasiliano
duniani biashara simu na posta hivi sasa ina ushindani mkubwa unaohitaji
mtazamo mpana wa kibiashara ili kukidhi mahitaji ya soko.
“Serikali inajitahidi kuisaidia TTCL na POSTA hivyo
wekezeni vizuri kwenye data na uharaka wa utoaji huduma ili muweze kushindana
kwenye soko na kukuza uchumi wa taasisi hizi muhimu kwa usitawi wa nchi”,
amesema Prof Mbarawa.
Prof. Mbarawa amezitaka menejimenti za POSTA na TTCL
kufanya kazi kwa uwazi na uadilifu ili malengo na mikakati ya taasisi hizo
yafahamike kwa wafanyakazi wote na kuwezesha kujipima kama wanafikia malengo
yaliyokusudiwa.
“Hakikisheni wafanyakazi wote wanaelewa malengo na
mikakati ya tasisi zenu ili kazi ya kuyatekeleza ifanywe kwa umoja na ushirikiano”,
amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amesisitiza umuhimu wa
wafanyakazi kuwa wadilifu na kuepuka kuwa mawakala wa mashirika mengine na
hivyo kuihujumu Serikali.
“kuna watu ndani ya TTCL na POSTA ambao ni wazembe,
wavivu na wanao hujumu Serikali tutawaondoa mara moja, Ni vema kubaki na
wafanyakazi wachache waadilifu kuliko wengi wasiotimiza maelngo
yaliyokusudiwa”, amefafanua Waziri Prof. Mbarawa
Naye Meneja wa TTCL mkoa wa Mwanza Bw. Johnbosco
Kalista amemweleza Waziri Mbarawa kuwa wigo wa mtandao kutofikia walaji wengi,
wateja kutolipa madeni kwa wakati na ulinzi na usalama wa miundombinu ya
mawasiliano ni miongoni mwa changamoto zinazoikabili shirika hilo mkoani
Mwanza.
Kwa upande wake Meneja wa POSTA mkoa wa Mwanza, Bw.
Julius Chifungo amebainisha kuwa uchakavu wa barabara, maslahi yasiyokidhi ya
wafanyakazi na uchakavu wa majengo ni miongoni mwa vikwazo vinavyoathiri
utendaji kazi wa shirika hilo mkoani Mwanza.
Takribani masanduku elfu tisa yanasimamiwa na Shirika
la Posta mkoani Mwanza katika ofisi zake kumi na moja na asilimia 96.8
hukodishwa na kuingizia shirika hilo faida, Wakati takriban wateja 45,041
wanahudumiwa na TTCL katika Mkoa wa Mwanza.
0 comments:
Post a Comment