WATANZANIA wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika Tamasha
la ‘Amsha Mama Tanzania’ linalotarajiwa kufanyika Machi 5 katika uwanja wa
Mwembeyanga Temeke jijini Dar es Salaam .
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa Kampuni ya Candy record yenye makao Mkuu yake nchini
Kenya ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo Joe Kariuki amesema wameamua kuleta
tamasha nchini ili kuwapa fursa akina mama wa Tanzania kujiinua kiuchumi .
“ Akina mama mjitokeze kwa
wingi katika tamasha hili mahususi kwenu kwa kuwa mtapata fursa mbalimbali na mtaweza kupata mambo
mbalimbali ikiwemo elimu,”alisema Kariuki.
Kwa upande wake balozi wa
Amsha Mama nchini Khalid Ramadhani (Tundaman), amewaomba wakinamama wachangamkie
fursa kwani watajifunza mambo mengi “Nawaomba Mama zangu mjitokeze kwa wingi
kwani tumepata bahati ya pekee ya kupendelewa kuletewa tamasha nchini kwani ni
adimu kutokea,” .alisema Tundaman.
Tamasha hilo linatarajiwa
kufanyika pia katika uwanja wa Ranchi ya Kedong uliopo jiji la Naivasha nchini
Kenya marchi 25-27 huku likitarajia kukutanisha akinamama kutoka nchi zote za Afrika
.
Aidha kutakuwa na burudani
kutoka kwa wasanii kama vile Juma Kassim
‘’Juma Nature’’, Khadija Kopa, Roma Mkatoliki, Young Killer, Msagasumu,
Man fungo, Sharo mwamba,Q-Chief,Mr Blue,Snura,Tundaman,na Ally Choki.
Tamasha la Amsha Mama
linatarajiwa kukutanisha akinamama mbalimbali kwa lengo la kujifunza kuhusu
kujikwamua kiuchumi kwani wao ndio chachu ya mafanikio.
Alisema wamejipanga
kuwapa radha tofauti watoto wa temeke na majirani zake ,hasa kwa
akina mama kupata fursa ya kujielewa na kujitambua hasa katika kuendeleza
familia zao.
0 comments:
Post a Comment