Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwasalimia wakazi wa Msamvu mjini Morogoro wakati akiwa njiani kuelekea
Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwasalimia wakazi wa eneo la Magole mkoani Morogoro
Msafara
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
ukipita katika eneo la Msamvu mjini
Morogoro kuelekea Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiangalia ukarabati unaondelea katika barabara kuu ya Morogoro-Dodoma eneo la
Kibaigwa . sehemu ya barabara hiyo inakarabatiwa chini ya usimamizi wa Wakala
wa Barabara nchini TANROADS. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiangalia ukarabati unaondelea katika barabara kuu ya Morogoro-Dodoma eneo la
Kibaigwa . sehemu ya barabara hiyo inakarabatiwa chini ya usimamizi wa Wakala
wa Barabara nchini TANROADS.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiangalia ukarabati unaondelea katika barabara kuu ya Morogoro-Dodoma eneo la
Kibaigwa . sehemu ya barabara hiyo inakarabatiwa chini ya usimamizi wa Wakala
wa Barabara nchini TANROADS.
********************
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
amewataka watu wote waliotelekeza Mashamba na Viwanda walivyouziwa na serikali,
kuhakikisha wanafufua mashamba na viwanda hivyo mapema iwezekanavyo, kabla
serikali haijavinyang'anya na kuwagawia wanaoweza kuviendesha.
Rais Magufuli ametoa maagizo hayo alipokuwa akizungumza na wananchi
waliosimamisha msafara wake njiani, wakati akisafiri kwa gari kutoka Dar es
salaam kwenda Dodoma.
Amesema mkoa wa Morogoro ulikuwa na viwanda vingi na mashamba mengi
makubwa ambayo kama waliouziwa wangeyaendeleza, yangezalisha ajira na kuongeza
uzalishaji wa bidhaa za viwandani na Mazao ya kilimo, lakini waliouziwa
mashamba na viwanda hivyo wameamua kutekeleza ama kubadilisha matumizi, huku
wengine wakitumia rasilimali hizo kuombea mikopo katika mabenki jambo ambalo
serikali yake haitalikubali.
"Kama nilivyowaahidi wakati wa kampeni na leo narudia, wote
walioamua kutumia mashamba na viwanda walivyouziwa na serikali kwa ajili ya
kuchukulia mikopo kwenye mabenki badala ya kufanya uzalishaji wavifufue haraka,
vinginevyo tutawanyang'anya" amesisitiza Rais Magufuli huku akishangiliwa
na wananchi waliomsimamisha katika eneo la Msamvu Mjini Morogoro.
Rais Magufuli pia amesimamishwa na kuwasalimu wananchi wa Wami Dakawa, Magole
na Dumila ambako pamoja na kuwahakikishia kuwa atatekeleza ahadi yake ya kuwapa
mashamba atakayonyang'anya kutoka kwa walioyatelekeza, amewataka kuachana na
migogoro kati ya wakulima na wafugaji na badala yake watatue migogoro hiyo kwa
kutumia njia za kisheria.
Aidha, amewataka viongozi wote wa Mkoa hadi vitongoji kushirikiana
kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji kabla haijasababisha madhara, na
ameonya kuwa migogoro hiyo ikileta madhara itakuwa ni kigezo tosha kuwa
viongozi hao wameshindwa kutekeleza wajibu wao na wanapaswa kuachia ngazi.
Pamoja na hayo Rais Magufuli amewahimiza wananchi hao kuchapa kazi kwa
juhudi hasa katika kipindi hiki ambacho mvua zinanyesha, na pia wahakikishe
kuwa watoto wote wanaopaswa kuandikishwa shule wanapelekwa shule, hasa baada ya
serikali kuamua kutoa elimu bure ya kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha
nne.
"Tumeamua kutoa elimu bure na tutatoa elimu bure, na jambo hili
limeonesha mafanikio makubwa kwa kuwa hata shule zilizotarajia kuandikisha
wanafunzi 45 zimejikuta zikiandikisha hadi wanafunzi 600 kwa darasa moja"
alibainisha Rais Magufuli.
Katika hatua nyingine Rais Magufuli amekagua kipande cha barabara kuu
ya Morogoro - Dodoma kilichoharibiwa na maji ya mvua katika eneo la Kibaigwa
Mkoani Dodoma, na kujionea kazi za ukarabati zinazofanywa na wakala wa barabara
nchini (TANROADS).
Amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa, kuongeza wakandalasi wa kukarabati eneo hilo ili kazi ikamilike haraka
badala ya kusubiri mpaka baada ya miezi miwili ilivyopangwa na wizara.
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kesho tarehe 06 Januari, 2016 atashiriki maadhimisho ya miaka 39 ya
kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), zitakazofanyika katika uwanja wa
Namfua, Mjini Singida.
0 comments:
Post a Comment