Nafasi Ya Matangazo

January 20, 2016

 Mkaguzi Msaidizi wa Polisi wa Dawati la Jinsia wilaya ya Kinondoni Inspekta Prisca Komba akitoa mafunzo ya jinsia kwa wafanyakazi wa kiwanda cha TBL Mbeya .Mafunzo haya yanaendelea katika viwanda vyote vilivyopo chini ya TBL Group nchini.
*****************
WAFANYAKAZI wa kampuni ya TBL Group katika kiwanda cha Mbeya leo wamepatiwa  semina kuhusiana na masuala ya jinsia na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi wa Dawati la Jinsia wilaya ya Kinondoni Inspekta Prisca Komba.

Katika semina hiyo wafanyakazi waliweza kujua masuala mbalimbali yanayohusiana na masuala ya kijinsia ambapo pia walipata fursa ya kuuliza sheria na masuala ya jinsia kutoka kwa mkufunzi huyo kutoka Jeshi la Polisi.

Baadhi ya wafanyakazi walioshiriki mafunzo hayo walisema kuwa yameweza kuwafumbua macho kujua masuala mbalimbali yatakayowasaidia katika maisha yao ya kila siku wanapokuwa sehemu za kazi na katika maisha ya kawaida na familia zao wanapokuwa wameishatoka kazini.
Inspecta  Prisca akiwazungukia washiriki wakati wa semina
 Baadhi wa wafanyakazi wa TBL Mbeya walipata fursa ya kuuliza maswali kwa Inspecta Prisca wakati huo huo wakipata chakula cha mchana.
Baadhi wa wafanyakazi wakiburudika na kupata maarifa baada ya saa za kazi wakati wa mafunzo hayo awamu ya jioni
Posted by MROKI On Wednesday, January 20, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo