Mwanzilishi
na mchapishaji wa jarida la Forbes Afrika, Bw. Rakesh Wahi ( wa pili
kushoto) akikamkabidhi Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania na Afisa
Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji (wa pili kulia)
tuzo ya Heshima Barani Afrika "2015 Forbes Africa Person of the Year"
iliyotolewa na Jarida la Forbes Afrika kwa kutambua mchango wake katika
kusaidia jamii ikiwemo kutoa ajira kwa zaidi ya watu 26,000 nchini na
mambo mengine yanayoigusa jamii. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Forbes Afrika, Sid Wahi (kulia) na MEC Panyaza Lesufi kutoka
kitengo cha elimu, Gauteng Province (kushoto).
Mfanyabiashara
maarufu ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group,
Mohammed Dewji akitembea kwenye 'Red Carpet' mara baada ya kuwasili
katika hotel ya Hilton Sandton jijini Johannesburg, Afrika Kusini kwenye
hafla ya utoaji tuzo iliyoandaliwa na jarida maarufu la Forbes na
kutunukiwa tuzo ya "Forbes Africa Person Of the Year 2015".
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akifurahi
jambo na baadhi ya wageni waalikwa nje ya ukumbi wa hafla hiyo ya utoaji
tuzo iliyoandaliwa na jarida la Forbes. PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akibadilishana
'Business card' na mmoja wa wageni waalikwa katika hafla hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji pamoja na ujumbe wake alioambatana nao kutoka Tanzania.
Sehemu
ya ujumbe kutoka Tanzania uliombatana na Afisa Mtendaji Mkuu wa
Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji kwenye hafla hiyo.
Burudani mbalimbali zikiendelea ukumbini hapo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Jarida la Forbes Afrika, Sid Wahi akitoa neno la ukaribisho
kwa wageni waalikwa. Kulia ni Head of Events wa ABN Productions,
Alexander Leibner.
Mfanyabiashara
maarufu nchini Tanzania na Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL
Group, Mohammed Dewji akitoa neno la shukurani baada ya kukabidhiwa kwa
tuzo, alisema anatoa tuzo hiyo kwa vijana wa Kitanzania kwani ndio nguvu
kazi inayobeba uchumi wa nchi.
MO
akiteta jambo na Mchumi mahiri raia wa Nigeria ambaye kwa sasa ni
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, Arunma Oteh (kulia) ambaye walikuwa
pamoja kwenye kinyang'anyiro cha kuwania tuzo hiyo ambapo pia
alimpongeza sana.
Pichani juu na chini MO akiendelea kupongezwa na wadau mbalimbali walioalikwa kwenye hafla hiyo.
Pongezi kwa MO zikiendelea kutolewa.
MO
katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Jaguar
Land Rover ambao ni miongoni mwa wadhamini wa sherehe za tuzo hizo.
MO katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Makampuni ya MeTL Group, Vipul Kakad mara baada ya kutwaa tuzo hiyo.
Makamu wa Rais wa MeTL GROUP, Vipul Kakad na Shemane Amin wakipitia moja ya taarifa iliyowavutia kwenye jarida la Forbes Afrika.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Jaguar Land Rover ya Afrika Kusini wakipozi kwenye 'Red Carpet'.
*************
Na Modewjiblog team
MFANYABIASHARA
na mtu mwenye taasisi ya kusaidia jamii, Mohammed Dewji maarufu kama
Mo ametunukiwa tuzo ya jarida maarufu la Forbes ya "Forbes Africa
Person Of the Year 2015" katika hafla iliyofanyika Novemba 27 mwaka huu
jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Mfanyabiashara
huyo pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises T
Ltd (MeTL Group) kampuni iliyoanzishwa na na baba yake katika miaka ya
1970 ambayo sasa imekua na kujikita katika viwanda vya nguo, usagaji
nafaka, utengenezaji wa vinywaji baridi, usindikaji wa mafuta ya kula,
usindikaji wa chai na kuendesha mashamba ya mkonge ambapo tayari
anashea ya asilimia 40 ya soko.
Mo
ametwaa tuzo hiyo kwa kuwashinda watu watano mashuhuri barani Afrika.
Watu hao ni Nkosazana Dlamini Zuma, mke wa Kwanza wa Rais wa Afrika
Kusini, Jacob Zuma. Mama huyo kwa sasa ndiye Mwenyekiti wa Umoja wa
Afrika (AU). Mwingine ni Rais wa sasa wa Nigeria, Muhammadu Buhari
aliyetambuliwa kutokana na kuanzisha vita dhidi ya rushwa nchini mwake.
Aidha
wapo Arumna Otei, mchumi mahiri raia wa Nigeria ambaye kwa sasa ni
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia. Pia alikuwemo Mwandishi maarufu wa
vitabu wa Nigeria, Chimanda Ngozi Adichie ambaye moja ya vitabu vyake
vinaelezea picha halisi ya Afrika inavyofikiriwa duniani.
Akitoa
neno la shukurani baada ya kukabidhiwa kwa tuzo hiyo Mo, alisema anatoa
tuzo hiyo kwa vijana wa Kitanzania kwani ndio nguvu kazi inayobeba
uchumi wa nchi.
Mo
ambaye kampuni yake ya MeTL inaongoza kwa kutoa ajira nchini, ikiwa
imetoa ajira 26,000 kote katika viwanda vyake 31 vilivyopo nchini na
katika mataifa matano ya Afrika, alisema amefurahishwa na tuzo hiyo
ambayo anaitoa kwa vijana kwa kutambua pia wajibu mkubwa walionao katika
kukabiliana na umaskini.
Alisema
ajira 26,000 zimegusa watu wengi nchini na kwamba ana matumaini
makubwa ya siku za usoni kutoa ajira zaidi kutokana na biashara zake
kuendelea kukua.
"Heshima
yangu kubwa haitokani na utajiri, maana kama utajiri wako hauna msaada
wala kugusa watu masikini hauna maana yeyote, hivyo basi heshima hii ni
kutokana na kwanza bidhaa zangu kugusa maisha ya watu kila siku kuanzia
sukari na majani ya chai asubuhi pamoja na unga wa ngano, lakini pia
chakula cha mchana kwa unga wa sembe, mafuta ya kupikia na maji ya
kunywa, bidhaa zote hizo za Mohammed Enterprises zinagusa maisha kila
nyakati katika siku.
"Nina
viwanda 31 ambavyo vimekuwa vikitengeneza bidhaa za Kitanzania na
kuziuza kwa Watanzania kwa bei yenye unafuu mkubwa, mathalani tunauza
maji kwa bei chini ya dola moja kwa shilingi za Kitanzania 200, hakuna
hata Ulaya, nina kiwanda cha khanga na vitenge ambacho malighafi zake
zote ni za Kitanzania, hivyo kuna kusaidia serikali kwa kulipa kodi
ipasavyo, lakini pia kusaidia moja kwa moja ajira za Watanzania walio
wengi ambao tatizo lao kubwa katika kundi la vijana ni ajira".
Alitumia
fursa hiyo kumshukuru na kumpongeza baba yake kwa kumwita mjasiriamali
shujaa ambaye alitoka kuanzia dereva wa malori baada ya kuhitimu kidato
cha nne mwishoni mwa miaka ya 1960 hadi kufikia ubilionea. Alisema
alipata maono ya utajiri hasa kutoka kwa baba yake huyo aliyekuwa
akimshirikisha biashara tangu akiwa mdogo.
“Mwanaume
mwenye ndoto huhitaji mwanamke mwenye maono. Na nimebarikiwa mwanamke
ambaye kwa miaka 15 amekuwa akinipa sapoti isiyoyumba.
“Saira,
nina shukurani nyingi kwako kwa kuwa nguzo ya familia yetu, mama wa
heshima kwa watoto wetu watatu,” alisema Mo kwenye hafla hiyo.
Kwa
utulivu, Mo alisema: “Baba, zawadi kubwa ambayo ulinipa katika maisha
yangu ni muda wako, na kwa hilo nitakuwa mwenye deni la shukurani kwako
siku zote za maisha yangu.”
Mo
ambaye moyo wake wa binadamu ulimfanya awanie uwakilishi Jimbo la
Singida Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kushinda nafasi
hiyo na hivyo kuwawakilisha wanasingida kuanzia 2005 na 2015 amesema
maisha ni changamoto kubwa inayobadilishwa kwa utumishi wenye nia ya
dhati kwa umma.
Alisema
alipowania uwakilishi alikuwa na sababu: “Nilikuwa na umri wa miaka 24,
nilikwenda Singida kutoa heshima kwenye kaburi la marehemu babu yangu.
Sikuwa nimefika huko tangu nilipoondoka nikiwa na umri wa miaka mitatu.
“Nilipokuwa
njiani, nilimuona mzee akiwa na maji yenye rangi ya njano, machafu
ambayo aliyatumia kwa kunywa. Nilishangaa, maana hali ile sikuwahi
kufikiri kama ipo vile. Kipindi hicho nilikuwa nimemaliza Chuo Kikuu cha
Georgetown, Marekani.”
Mo
anasema kuwa aliingiwa na hisia kutaka kujua nini hasa alichokuwa
anahitajika kufanya, alimfuata yule mzee aliyekuwa na maji yale,
alipozungumza naye, aliwazungukia watu wengine na kuridhika kuwa ile
ndiyo hali halisi, hapo ndipo fikra ya kwa nini agombee ubunge
ilipoanzia.
Anasema
kuwa baada ya kujiridhisha hivyo, alirudi kwa mzee wa kwanza,
alizungumza naye na kumuuliza ni kwa nini shida ile ilikuwa haizungumzwi
kwa upana katika mamlaka husika.
“Nilipojitambulisha yule mzee alisema anamkumbuka babu yangu, kisha
akanishauri nigombee ubunge, alinisisitiza mno ili nisaidie kuondoa lile
tatizo la watu wa Singida kunywa maji machafu,” alisema Mo.
Anaeleza
kuwa alipokuwa njiani kurejea Dar es Salaam, alilifikiria tatizo hilo
kwa mapana zaidi, akalifanyia utafiti na kubaini kwamba katika kila watu
10, watatu walikuwa wakipoteza maisha kutokana na maradhi
yanayosababishwa na maji machafu.
Anaendelea
kusema kuwa aligundua kuwa Singida kulikuwa na tatizo kali la maji safi
na salama. Anasema kuwa alibaini uwepo wa tatizo la elimu kuhusu
matatizo ya maji.
Jambo lingine ambalo anasema aliligundua ni uwepo wa tatizo la huduma za afya.
“Niliwafikiria
watoto wangu, jinsi ninavyowapenda, na namna ambavyo kila mzazi
anavyompenda mwanaye. Nilipingana na hali kuwa watoto wa Uingereza na
Marekani wamependelewa zaidi. Maisha ni sawa bila kujali chochote,”
anasema Mo.
“Niliona
lazima nitimize wajibu wangu. Kutimiza malengo yangu ya kusaidia jamii,
kufanikiwa katika biashara. Mambo hayo mawili hisani na biashara
nimeyaweka pamoja na ndiyo maana nimefika hapa leo, tunajivunia sana
kuitwa METL nembo ya Watu.
Katika
miaka yangu 10 kama mbunge, nimefanya mabadiliko mengi, Nilikuwa na
sababu ya kupata mkopo nafuu wa dola milioni 35, ambao ulisababisha
kuwekwa kwa miundombinu ya maji safi na salama Manispaa ya Singida.
“Niliitumia
MeTL, tuliweza kudhamini shughuli nyingi za maendeleo ya kijamii.
Kuhusu elimu, nilifanikisha kujenga shule 15, zikawa 17, kabla ya hapo
tulikuwa na shule mbili tu.
“Kuhusu
huduma za afya, hapa nimshukuru mke wangu kwa jitihada zake. Alikuwa
Mwenyekiti wa taasisi ya Tumaini la Maisha ambayo imekuwa ikisaidia watu
wengi, hasa watoto dhidi ya maradhi ya saratani.”
0 comments:
Post a Comment