Nafasi Ya Matangazo

November 05, 2015


Na Father Kidevu Blog,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk John Pombe Magufuli  amemteua  Bwana George Mcheche Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.



Akizungumza na waandishi wa habari Ikulu, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amesema Rais Dk.John Magufuli ameyafanya uteuzi huo, katika siku yake ya kwanza ya kuingia ofisini Ikulu jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo. 


Itakumbukwa kuwa , Ijumaa, Januari 2, 2015 huu Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alimteua Masaju kushika wadhifa huo kwa mara ya kwanza baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwanasheria wa Serikali, Jaji Fredrick Werema.



Mwanasheria Mkuu huyo ataapishwa kesho Ijumaa Novemba 6, 2015, Ikulu, Dar Es Salaam.



Masaju  alipata kuwa mshauri wa Sheria wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na baade kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali .



Katia hatua Nyingine, Rais Dk John Pombe Magugufuli  ameitisha Bunge la 11 ambapo wabunge watakutana mjini Dodoma Novemba 17 na Novemba 19 atapeleka jina la Waziri Mkuu ambae atamteua kwa ajili ya kuidhinishwa na Bunge hilo.
Posted by MROKI On Thursday, November 05, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo