TABIANCHI YAWEKA HIFADHI ZA TANZANIA HATARINI
Na Andrew Chale, modewjiblog
[TANZANIA] Zimebaki siku zaidi ya 60, kuelekea mkutano mkuu wa 21 (COP21) wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Nchi (UNFCCC) unaotarajiwa kufanyika Paris, Ufaransa. mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka huu.
Dulu na chunguzi za kitafiti zinaeleza kuwa, Tanzania ni miongoni mwa Mataifa Barani Afrika yatakayokumbwa na janga kubwa dhidi ya Mabadiliko ya tabianchi (Climate Change in Tanzania National Parks) kwenye Hifadhi na mbuga zake.
Dulu hizo za kitafiti pia zinabainisha kuwa, asilimia kadhaa za Wanyama nao watatoweka kabisa hali ambayo taifa litakumbwa na matatizo mbalimbali ikiwemo kushuka kwa uchumi wa Nchi katika siku za usoni.
Hivi karibuni, mwandishi wa Makala haya wa modewjiblog, alipata kutembelea Hifadhi kadhaa za taifa zilizo chini ya usimamizi wa Shirika la Hifadhi la Taifa, Tanzania National Parks Authority (TANAPA). Hifadhi hizo zikiwepo Udzungwa, Selous Game Reserve, Mikumi, Ruha, na Saadan pamoja na kuonana na wataalamu wa mabadiliko ya tabianchi kwenye idara za serikali na watu binafsi. SOMA ZAIDI modewjiblog.com
0 comments:
Post a Comment