Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso akishiriki kupaka rangi katika darasa la Chekechea linalokarabatiwa kwa hisani ya Wafanyakazi wa Airtel kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Kumbu Kumbu iliyopo Block 41, jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia ni Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule hiyo, Joyce Mtanga (wa pili kulia) na Mwalimu, Flossy Mbwilo.
Wafanyakazi
wa Airtel Tanzania, Kitengo cha Mawasiliano na Raslimali Watu wakishiriki
kupaka rangi katika darasa la Chekechea linalokarabatiwa kwa hisani ya
Wafanyakazi wa Airtel kama sehemu ya
huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Kumbu Kumbu iliyopo Block 41, jijini
Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso akiupamba ukuta kwa kiganja cha mkono
kilichopakwa rangi nyekundu wakati waliposhiriki kupaka rangi darasa la
Chekechea linalokarabatiwa kwa hisani ya Wafanyakazi wa Airtel kama sehemu ya
huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Kumbu Kumbu iliyopo Block 41, jijini
Dar es Salaam jana. Wanashuhudia (kutoka kulia) ni Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule
hiyo, Joyce Mtanga, Mwalimu, Flossy Mbwilo na Afisa Uhisiano na Matukio wa
Airtel, Dangio
Wafanyakazi wa Airtel kupitia
Mradi wake wa Airtel “Tunakujali” waendelea kuchangia Maendeleo katika Jamii. Kwa hakika, safari ya maili elfu huanza na
hatua. Mradi ulioanza mwaka mmoja uliopita katika Shule ya Msingi ya Kumbukumbu
sasa tunaona matunda yake kwa kuona maendeleo yaliyopo katika shule ya msingi Kumbukumbu
iliyopo Kinondoni jijini Dar Es Salaam. Hii yote ni kwa hisani ya wafanyakazi
wa kitengo cha Rasilimali watu na kitengo cha mawasaliano kwa kufanya matembezi
ya Hisani mwaka jana kwa ajili ya kusaidia shule hiyo.
Wafanyakazi wa Airtel mwishoni mwa wiki iliyopita waliungana pamoja katika harakati za mwisho za kukarabati darasa la awali katika shule ya msingi ya Kumbukumbu. Shule hiyo ni miongoni mwa shule ambazo zipo katika mradi wa Airtel “Tunakujali”, ambapo Airtel wamekuwa wakizisaidia shule mbali mbali hapa nchini. Mwaka jana wafanyakazi wa Airtel walikabidhi kisima cha maji safi na salama katika shule hiyo.
Awali shule hiyo haikuwa na maji, ambapo wanafunzi na walimu walipata tabu na kuwawia ugumu wa kupoteza muda wa masoma kwa kutafuta maji. Wakiwa katika makabidhiano ya kisima hicho alishuhudia ubovu wa darasa la chekechea na watoto hao kukaa, hivyo walitoa ahadi ya kukarabati darasa hilo na kuwapatia madawa. Unapotoa ahadi japo sio shurti ni wajibu kuitekeleza, na kutokana na umuhimu huo Wafanyakazi wa Kampuni ya simu ya Airtel waliamua kutimiza dhamira yao na kuanza mchakato wa kukarabati darasa hilo kupitia mradi wao wa Airtel “Tunakujali”. Airtel "Tunakujali" ni miongoni mwa miradi ya kijamii inayoondeshwa na wafanyakazi wa Airtel ili kuweza kusaidia jamii inayowazunguka.
0 comments:
Post a Comment