MGOMBEA jimbo la Monduli kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Namelok Sokoine, akihutubia mkutano wa hadhara wakati wa
uzinduzi wa kampeni zake zilizofanyika katika viwanja vya Nanja Mnadani Monduli
mkoani Arusha Septemba 28,2015 ambapo pamoja na mambo mengine ameahidi
kuendeleza yote aliyoasisi, kusimamia na kutekeleza aliyekuwa mbunge wa jimbo
hilo, Edward Lowassa.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro akihutubia mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli Mkoani Arusha kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Namelok Sokoine.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Namelok Sokoine akihutubia wananchi katika mkutano huo wa hadhara wa uzinduzi wa kampeni zake.
Namelok Moringe Sokoine akiwasili katika uwanja huo wa Nanja tayari kwa uzinduzi wa kampeni.
Wazee wa Kimila wa Jamii ya Kimaasai wa Monduli wakiongoza dua maalim ya kumuombea Binti yao Namelok.
Mwalimu Lorinyu Nkoosi, mmoja wa waliochuana na Namelok Sokoine katika mchakato wa uteuzi ndani ya CCM akiongea.
Wananchi wa Monduli wakiwa katika mkutano huo.
Wajane
wa Waziri Mkuu wa Zamani wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine ambao ni
mama za Namelok Sokine wakitambulishwa mkutanoni hapo na Mwenyekiti
wa kamati ya kampeni za CCM jimbo la Monduli, Paul Kiteleki.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro (kulia) akimkabidhi ilani ya Chama cha Mapinduzi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli Mkoani Arusha kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Namelok Sokoine wakati wa uzinduzi wa jkampebni zake uliofanyika Monduli jana.
Dk Asha-Rose Migiro akisalimiana na wamama wa kimaasai alipowasili mkutanoni hapo.
0 comments:
Post a Comment